Naibu
Katibu Mkuu CCM Bara Mh:Mwigulu Nchemba akizungumza na Wananchi wa kata
ya Ifakara wakati wa Mkutano wa Kufungua Kampeni uliofanyika Jana
Tar.27/02/2014.Hapa akiwa na Wahanga wa siasa chafu zinazodaiwa Kufanywa
na
Chadema kupitia Vijana wake wa Redbrigade.Mwenye T-shirt ya Njano ni
Mzee Alphonce John ambaye alitopolewa Macho kwa dispisi wakati wa
Uchaguzi wa Udiwani huko Kahama Mwezi uliopita.
Mwigine
mwenye Shati la Kijana ni Kijana Musa Tesha ambaye alimwagiwa Tindikali
na Vijana wanaodaiwa Kuwa wa Chadema huko Igunga wakati wa Uchaguzi
Mdogo wa Jimbo hilo.
Mh:Mwigulu
Nchemba jana amesisitiza Wananchi wa Kalenga kuwa makini na siasa Chafu
za Chadema zinazofanywa sehemu mbalimbali hasa kwenye nyakati kama hizi
za Uchaguzi.Amesisitiza kuwa kwenye Chaguzi zozote Vyama vya siasa
vinashindanisha Sera na hoja kuhusu Maendeleo ya Wananchi wa eleo
hilo,Mkataba wa CCM na Wananchi ni Maendeleo katika Taifa hili,Umoja na
Mshikamano ndio ngao ya MwanaCCM yeyote.
Mwigulu Nchemba amesema dhambi ya Mauaji na Unyama unaoendelea kwenye mikutano ya siasa na maeneo mbalimbali haitamwacha Dr.slaa Salama kutokana na yeye kuwa kiongozi anayebariki Siasa chafu hizo.
Chanzo:Kalenga
2 comments:
Hizi ni Siasa chafu za CCM kutembeza wagonjwa wanaodaiwa kuumizwa na CHadema ambayo sio kweli kisa kutafuta kuchukua jimbo la Kalenga huu ni uhuni r Nchemba. Tafuteni nafasi kwa ukweli wa nini mnawafanyia wananchi. Hao mtawatembeza hadi lini. Hamna la kuwaambia wananchi wanaotaabika na mali zao. Maji masafi hawana, barabara mbovu, shule na hospitali hakuna vitanda. Hii ni aibu tosha. CCM mnaimaliza Tanzania.
ccm ndo yenye siasa chafu tena wao ndo wanaofanya matukio halafu wanawasingizia wanasiana wa upinzani wadanganyika kaeni mmkijua kila mnapoichagua ccm na ndo kila mtakapo kuwa walalahoi daima.
akili ni mali tumeyeni akili zenu wadanganyika wenzangu
Post a Comment