Wakuu
wa Majengo wakiwa na vyeti vyao mara baada ya mafunzo. Waliokaa kuanzia
kushoto ni Bw. Godfred Mbanyi mwezeshaji kutoka Bodi ya Watalaam wa
Ununuzi na Ugavi, akifuatiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya
Taifa Muhimbili Dkt. Marina Alois Njelekela, Dkt. Clemcence Tesha ambaye
ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Watalaam wa Ununuzi na Ugavi
akifuatiwa na Bi. Agnes Mtawa ambaye ni Mwenyekiti wa Tenda Bodi ya
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wakuu
wa Idara mbalimbali za Hospitali wakiwa na vyeti vyao mara baada ya
mafunzo. Waliokaa kuanzia kushoto ni Bw. Godfred Mbanyi mwezeshaji
kutoka Bodi ya Watalaam wa Ununuzi na Ugavi, akifuatiwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Alois Njelekela,
Dkt. Clemence Tesha ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Watalaam
wa Ununuzi na Ugavi akifuatiwa na Bi. Agnes Mtawa ambaye ni Mwenyekiti
wa Tenda Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Wakurugenzi
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakiwa na vyeti vyao mara baada ya
mafunzo. Waliokaa kuanzia kushoto ni Bw. Godfred Mbanyi mwezeshaji
kutoka Bodi ya Watalaam wa Ununuzi na Ugavi, akifuatiwa na Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Alois Njelekela,
Dkt. Clemence Tesha ambaye ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Watalaam
wa Ununuzi na Ugavi akifuatiwa na Bi. Agnes Mtawa ambaye ni Mwenyekiti
wa Tenda Bodi ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Viongozi
wa Hospitali ya Taifa Muhimbili ambao ni Wakuu wa Idara, Mameneja wa
Majengo, pamoja na baadhi ya Wakuu wa Vitengo vya Tiba ya Figo na
Magonjwa ya Mtumbo wamepigwa msasa kuhusu menejimenti ya usimamizi wa
Idara na Vitengo wanavyoviongoza. Wakuu hawa wa Idara na Mameneja wa
Majengo wamechukua nafasi hizi mapema mwezi Januari 2014 zitakazodumu
kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Mafunzo
haya yalikuwa na mada kadhaa ikiwemo wajibu wa Wakuu wa Idara na
Mameneja wa Majengo, Mawasiliano Rasmi ndani na nje ya Taasisi,
Umuhimu na namna ya kufanya Tathmini kwa wafanyakazi walioko chini yao,
mipaka yao katika kufanya kazi, namna ya kutengeneza mpango kazi wa
mwaka uliotoolewa kwenye Mpango Mkakati wa Hospitali, jinsi ya kutoa
adhabu kwa wafanyakazi pamoja na utaratibu unaotakiwa kufuatwa.
Aidha,
Viongozi hawa walipata mafunzo kuhusiana na kanuni za fedha, utaratibu
wa kuandaa bajeti na malipo, umuhimu wao katika kubuni vyanzo vya
mapato na kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha, umuhimu wa kusimamia
watendaji walioko chini yao ili kujaza kwa usahihi fomu mbalimbali za
matibabu ya wagonjwa ikiwemo fomu za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na
bima nyinginezo.
Mada
nyingine ilihusu matumizi ya teknolojia ya habari na mawasiliano ambapo
Hospitali ya Taifa Muhimbili inatakiwa kuacha matumizi ya karatasi
(paper less) ili kuwa mfano kwa Hospitali nyingine za umma hapa nchini.
Viongozi
hawa walipata mafunzo pia kuhusiana umuhimu wa mawasiliano kati yao
viongozi kwa viongozi, kati yao na wafanyakazi walioko chini yao na
kikubwa zaidi umuhimu wa kuwasiliana na wateja wanaowahudumia ili
kuhakikisha wanawapata taarifa sahihi kuhusu mienendo ya matibabu yao.
Aidha
walipata fursa ya kujua utaratibu unaotumika katika kufanya manunuzi ya
vifaa tiba, dawa pamoja na vitendanishi mbalimbali kwa ajili ya matumizi
ya Hospitali katika idara wanazoziongoza.
Kimsingi
Viongozi hawa wanatoka katika Kurugenzi nane za Hospitali ya Taifa
Muhimbili ambazo ni Kurugenzi ya Tiba yenye Idara saba ambazo ni (Idara
ya Tiba, Magonjwa ya Dharura, Afya ya Watoto, Utengamano, Magonjwa ya
Nje, Idara ya Magonjwa ya Afya ya Akili, na Idara ya Magonjwa ya Moyo
ambayo ni idara mpya ikijumuisha kitengo cha upasuaji wa moyo).
Kurugenzi
ya Upasuaji yenye Idara sita ambazo ni (Idara ya Upasuaji ikijumuisha
Kitengo cha Upasuaji wa Watoto, Nusu Kaputi na Kitengo cha Wagonjwa
Mahututi (ICU), Macho, Idara ya Afya ya Kinywa na Meno, Magonjwa ya
Akina na Mama na Uzazi pamoja na Idara ya Pua Masikio na Koo.
Kurugenzi
ya Tiba Shirikishi ina Idara tatu ambazo ni (Idara ya Radiolojia,
Famasi na Idara ya Maabara ikijumuisha Chumba cha Kuhifadhi Maiti
(Mortuary).
Kurugenzi
ya Uuguzi ina idara nne ambazo ni (Idara ya Utasishaji,Huduma za
Chakula, Idara ya Uuguzi na Utunzaji wa Majengo, na Ustawi wa Jamii.
Kurugenzi
ya Utumishi ina Idara mbili ambazo ni (Idara za Ajira na Mafunzo na
Idara ya Maslahi ya Watumishi). Kurugenzi ya Ufundi ina idara mbili
ambazo ni (Idara ya Ufundi na Idara ya Mazingira).
No comments:
Post a Comment