Mkali wa Mduara anayewakilisha pande za Zanzibar, AT.
MKALI wa Mduara anayewakilisha pande za Zanzibar, AT amesema kuhusiana na ishu ya madai inayomkabili, ameiachia mahakama hivyo kila kitu kitaeleweka huko.
Machi 10, mwaka huu AT alipandishwa katika Mahakama ya Mwanzo ya Buguruni kujibu kesi iliyofunguliwa na jamaa mmoja anayejulikana kwa jina la Salum Abdallah ambaye anadai alikuwa ni mganga ambaye anasema anamdai msanii huyo Sh Mil. 3.
Imeelezwa kuwa, mganga huyo anamdai fedha hizo kama ujira wake baada ya kumtibia tatizo lake la kumpandisha nyota na kumsaidia ashinde Tuzo za Kill Music mwaka 2013.
Akionesha msimamo wake katika jambo hilo, AT alisema hana cha kuzungumza juu ya ishu hiyo lakini ukweli utadhihirika mahakamani.
“Suala limeshafika mahakamani, April 2, mwaka huu tutarudi tena kwa ajili ya kutolewa ushahidi, kitaeleweka tu,” alisema AT.
Vijimambo baada ya kusoma habari kotoka GPL ilimvutia waya AT na hiki ndicho alichozungumuza

No comments:
Post a Comment