jinsi ya kushiriki.
kuchagua bidhaa.
hundi.
Nadhir akimkabidhi hundi mshindi.
Na Andrew ChaleKAMPUNI ya uuzaji wa bidhaa za majumbani na ofisini ya Home Shopping Centre (HSC) imemzawadia
mshindi wake wa kwanza wa ‘pendezesha nyumba na HSC’ Rehane Jaffer hundi ya sh 500,000.
Shindano hilo linaendeshwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook na limepewa jina la‘Give a Way’.
Hundi hiyo ilikabidhiwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Mauzo na Masoko wa HSC, Nadhir Mubarak Bahayan ambaye aliwataka watanzania kushiriki shindano hilo ambalo kila Ijumaa
watakuwa wakijishindia sh. 500,000.
“Wateja wetu wa HSC, wanatakiwa kujiunga kwenye mtandao wetu wa facebook na
kisha kututumia picha walizopamba ndani ya nyumba zao zitokanazo na bidhaa zetu,” alisema Nadhir.
Alisema shindano hilo litaendeshwa kwa mwezi mzima wa Machi. Mshindi huyo aliipongeza
HSC kwa shindano hio na kusema ni faraja kwake na familia yake.
Aidha zoezi hilo ambalo litaendeshwa kwa muda wa mwezi mzima wa Machi huku kila Ijumaa ikitarajiwa kutangaza washindi na kukabidhiwa hundi siku inayofuata.
Nadhir aliwataka wateja wao kuwa natabia ya kutembea kwenye mtandao wa HSC, na kushiriki
kupitia https://www.facebook.com/hsctz





No comments:
Post a Comment