ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 14, 2014

Taarifa ya uteuzi wa viongozi wa Bodi ya PUMA Energy

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA NISHATI NA MADINI

TAARIFA YA UMMA

UTEUZI WA MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI YA PUMA ENERGY (T) LTD NA WAKURUGENZI WA BODI
 
Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, amemteua Dkt. Ben E. Moshi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya PUMA Energy (zamani ilijulikana kama BP Ltd). Uteuzi huo wa Dkt. Ben Moshi ni wa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 1 Machi, 2014.
 
Kutokana na uteuzi huo Waziri wa Nishati na Madini, Mhe. Profesa Sospeter M. Muhongo (Mb.)
amewateua wafuatao,
kuwa Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya PUMA Energy (T) Ltd kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 1 Machi, 2014:
  1. Mhandisi Dkt. Malima MP. Bundara, Mwenyekiti Mtendaji wa Kituo cha GARETRACE;
  2. Bw. Solomon R.M. Odunga; Katibu Mkuu Mstaafu;
  3. Bw. James Andilile, Kamishna Msaidizi wa Nishati katika Wizara ya Nishati na Madini; na
  4. Bw. Daniel N. Nsanzugwanko, Mtaalam Mshauri wa masuala ya biashara.
Imetolewa na
KATIBU MKUU

No comments: