Msanii
wa Kizazi Kipya (Bongo Fleva) Ndugu Haji Noorah ambaye Kimziki/Sanaa
anafahamika kwa Jina la Noraah A.K.A Baba Stylez(Starz) akizungumza na
Vyombo vya Habari kuhusiana na Mwenendo wa Afya Yake.Habari Kwanza Blog
imekutana na Msanii Noorah kujua hali ya Afya yake"Kimsingi naendeea
Vizuri kwa sasa,Nilikuwa nimelazwa Hospitali ya Kairuki(Mikocheni
Mission Hospital) kwa tatizo la Tumbo,Nimekuwa nikizumbuliwa na Tumbo
kwa Muda wa miaka 20 nikidhani ninatatizo la Vidonda vya tumbo kumbe
ndivyo Sivyo,Baada yaVipimo vya Madaktari wamegundua ninatatizo kwenye Utumbo wangu,hivyo wameshaanza kunifanyia Matibabu na hali yangu imeendelea Kuimarika kadri ya siku zinavyo kwenda".Alisema Noorah.
Hit
Maker wa Lugha Gongana Noraah anaongeza "Rai yangu kwa Watanzania na
Wasanii wote tuwe na tabia ya Kufanya Uchunguzi wa Afya Zetu,Mimi
nimekuwa na tatizo hili kwa Muda wa miaka 20 nikidhani ni tatizo la
kawaida tu,baada ya kupima nimegundulika na tatizo kwenye Utumbo
wangu,nashukuru Mungu sana Madaktari wamefanya kazi kupitia Operesheni
ya Tumbo,hivi sasa naendelea Vizuri".
Noorah
amewashukuru sana Wasanii wote na Watanzania wanaoendelea kumuombea na
kumjulia hali yake,Hii inaonesha ni nanma gani Wasanii tunatakiwa kitu
kimoja wakati wa Shida na Raha.
Rais
wa Shirikisho la Muziki Tanzania Ndugu Addo Novemba Mwasongwe
akizungumza na Vyombo vya habari mara baada ya Kuwasili na Ujumbe wake
Nyumbani kwa Msanii Noorah kwaajili ya Kumjulia hali yake na kutoa
mchango wao kwaajili ya Afya ya Msanii Noorah.Addo Tanzania amesisitiza
Umoja miongoni mwa Wasanii wakati wote,Shirikisho linaomba Wasanii
kusaidiana katika Shida na Raha,"Tumekuaja kumuona Noorah kwasababu ni
Mwanamuziki Mwenzetu na amekuwa bega kwa bega kwenye sanaa
yetu,Shirikisho linatoa Rai kwa Wasanii na Watanzania kuja kumuona
Msanii mwenzao hapa Nyumbani,kumjulia hali na hatimaye Uwe utamaduni
wetu kwa Wasanii wote tunapopatwa na Matatizo."Alisema Addo.
Makamu
wa Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania Ndugu Samwel Braiton
alimaarufu Braiton Mtz na Mmiliki wa Backyard Reckords akizungumza na
Vyombo vya Habari nyumbani kwa Msanii Noorah hii leo alipofika kwaajili
ya Kumjulia hali.Kubwa zaidi Braiton amewaomba Wasanii kujenga Utamaduni
wa Kusaidiana na Kujuliana hali,haitakuwa afya sana hadi mtu apate
tatizo kubwa sana ndipo watu waanze kujitokeza"Nawasanii Wasanii wote
tuungane katika hali yoyote na tujenge utamaduni wa kujuliana hali". 
Rais
wa Shirikisho la Muziki Tanzinia Ndugu Addo Novemba Mwasongwe
akikabidhi Mchango wa Fedha Taslimu Laki tano kwa Msanii Noorah hii leo
walipofika Nyumbani kwake kwaajili ya Kumjulia hali yake ya Kiafya.
Ujumbe
kutoka COSOTA,Kushoto ni Philemon Kila Ofisa Msajili wa Umiliki kazi za
Wasanii,katikati Msanii Noorah na Kulia ni Ofisa kutoka COSOTA
anayeshughulikia Teknolojia na Mawasiliano.
Hapa
ni Mkurugenzi wa Habari Kwanza Media/Blog Ndugu Sanga Festo akiwa
katika Picha ya pamoja na Msanii Noorah baada ya Kumtembelea Nyumbani
kwake Sinza-Darajani hii leo.
Hivi
Sasa Noorah anaendelea na Matibabu katika Hospital ya
Mikocheni(kairuki) kwa mfumo wa Kliniki na anatarajia kuhudhuria Kliniki
baada ya wiki mbili kaunzia sasa.Jumla ya Gharama zake za Matibabu hadi
sasa zimefikia Milioni 2.7,Wasanii/Watanzania mnaomba kuungana na kutoa
sapoti yenu kwa ndugu Yenu na Msanii wenu Noorah katika kipindi hiki
cha Kurejesha afya yake katika hali ya kawaida iliaendelee na majukumu
ya Kila siki katika sanaa na Maisha yake binafsi.
Picha na Habari kutoka kwa Sanga Festo wa Habari kwanza Media/blog
No comments:
Post a Comment