ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, March 29, 2014

Wanajeshi JWTZ wanaendelea kuwapa mashaka wananchi wa Kimbiji, Dar-es-salaam

Hali ya wasi wasi na maisha ya mashaka yanayosababishwa na uvunjwaji wa haki za binadamu unaofanywa na kikosi kimoja cha jeshi la wananchi JWTZ unazidi kuwapa kero wananchi wa maeneo ya Kimbiji,wilayani Temeke,Dar-es-salaam. Kutokana na kuvamiwa na wanajeshi katika makazi na maeneo yao ya ardhi,ambapo wanajeshi wanawalazimisha wananchi waondoke
bila ya ridhaa yao, wala kufuata misingi na taratibu za sheria za
ardhi.

Baadhi ya wanajeshi wamekuwa wakiweka mahema nje ya makazi ya raia hao na kuwapa usumbufu familia za raia hao wakiwemo akina mama na watoto. Pamoja na wananchi wa Kimbiji kulalamika mara nyingi katika vyombo vya habari ,pia katika vyombo serikali kuhusu majanga
haya, cha kusikitisha hakuna jibu lolote walilo pewa ! Wananchi wa Kimbiji wanasikitishwa sana na usumbufu wanao upata kutoka kwa wanajeshi JWTZ ambao wanadhamana ya kulinda nchi
sio kuwanyanyasa wananchi bila ya kufuata misingi ya sheria za miliki ardhi,wakati serekali nayo haijatoa tamko lolote kuhusu unyanyaswaji huo.


Wananchi wa Kimbiji wanamiliki maeneo yao ya asili na hawajawai kushiriki katika kikako chochote kile kinachohusu kugawa maeneoau kupisha mradi wowote ule wa maendeleo na Jeshi  JWTZ. Wananchi wa Kimbiji wamedai kuwa wanajeshi wana lengo la kuwapora
Ardhi kwa kutumia vitisho vya kofia na nembo ya JWTZ. wananchi wanaiomba serikali pamoja tahasisi za mbali mbali kuingilia kati na kulitafutia ufumbuzi tatizo hili linalo wanyima usingizi
wananchi wa Kimbiji. kwa maelezo zaidi wasiliana na uongozi wa kimbiji
Simu: 0713768082 Diwani au 0713846688 Mwenyekiti

1 comment:

Anonymous said...

SASA HAWA WANAJESHI WAMEINGIA KWENYE KAZU HIYO YA KULINDA RAIA NA TAIFA LAKE SIO KUNYANYSA RAIA,NDANI YA NCHI YAO WANASAHAU WAJIBU WAO, AU HAWAJAPATA DARASA VIZURI LA KUJIELEWA WAPO HAPO KAZINI KWA SSABABU GANI? MANAKE MAMBO HAYA NI AFRICA TU KWA AJILI YA UKOSEFU WA ELIMU YA KUTOSHA