| Walikuwa na sababu ya kuwa mabingwa na hii ndiyo darasa tosha kwa timu zote za VPL kujifunza kutoka AZAM. Kwani ni Timu pekee yenye mfumo enderevu na mipango madhubuti kwa kuwa na kila kitu kinacho wafanya wachezaji wajisikie wapo nyumbani. Simba na Yanga zitabakia jina tu na kisiwa cha migogoro kutokana na viongozi figisufigisu na wanachama mbumbu wanaokumbatia viongozi wabovu baada ya kupewa kilo moja ya maharage na sembe. |
1 comment:
Ni kweli kabisa, kuikumbatia Simba au Yanga ni kuua mpira wa Tanzania. Timu hazina mfumo wa maendeleo kisoka kazi kukuza uchawi tu na kuua vipaji vya wachezaji wenzao.
Post a Comment