Band la Tanzania jana Jumamosi, April 26, 2014 lilikuwa kivutio kikubwa kwa wageni waliotembelea kwenye tamasha la Global Language Network (G- Festival) mjini Washington DC. Tanzania iliwakilishwa na Jumuiya ya Watanzania DMV ikishirikiana na Darasa la Kiswahili katika kuitangaza lugha ya Kiswahili, mavazi ya Kitanzania, mila na desturi zetu pamoja na vyakula vyetu.
Uongozi wa Jumuiya uliwakilishwa na Katibu wa Jumuiya, Bwn Amos Cherehani, Makamu Rais, Bwn Raymond Abraham na Mweka Hazina wa Jumuiya , Bwn Genes Malasy pamoja na walimu wa Darasa la Kiswahili, Ms Iris Zelske, Ms. Cechelela Tomi na Mwl Mkuu Lucia Mkumbukwa ambaye alisimamia idara ya vyakula vya Kitanzania.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
1 comment:
akiwa mzungu ndo watu wanakuja na kusikika si mnaona wenyewe katika hii picha
Post a Comment