Advertisements

Thursday, July 31, 2014

Nonga awachenjia wachezaji wa kigeni

Timu ya Mbeya City anayochezea Nonga ndiyo timu pekee ambayo haina mchezaji wa kigeni kati ya timu nne zilizomaliza katika nafasi nne za juu msimu uliopita na mpaka sasa haijaonyesha nia ya kusajili mchezaji yeyote kutoka nje ya nchi na kumfanya straika huyo kuamini kuwa wazawa wanaweza kufanya vizuri bila wageni.

STRAIKA wa Mbeya City, Paul Nonga amesema wachezaji wa kigeni wanaocheza mpira hapa nchini wengi wao ni mizigo kwani wameshindwa kucheza kwa viwango vya juu kama inavyotarajiwa na kumtaja Muivory Coast, Kipre Tchetche kuwa ndiye anayeonyesha uwezo wa juu mpaka sasa.


Timu ya Mbeya City anayochezea Nonga ndiyo timu pekee ambayo haina mchezaji wa kigeni kati ya timu nne zilizomaliza katika nafasi nne za juu msimu uliopita na mpaka sasa haijaonyesha nia ya kusajili mchezaji yeyote kutoka nje ya nchi na kumfanya straika huyo kuamini kuwa wazawa wanaweza kufanya vizuri bila wageni.


Nonga alisema kuwa wachezaji wa kigeni wamekuwa wakichota fedha nyingi kwenye klabu mbalimbali nchini lakini wameshindwa kuleta changamoto zozote na wakati mwingine kugeuka kuwa mizigo katika klabu zao.


Kwa nyakati tofauti klabu za Simba na Yanga zimekuwa zikiingia vitani kupambana na wachezaji wao wa kigeni ili waweze kuripoti kwenye mazoezi ya timu hizo pindi wanapopewa ruhusa ya kwenda makwao. Hivi karibuni Mkenya Donald Mosoti na Mganda Joseph Owino wa Simba walionyesha utovu huo wa nidhamu kwa kushindwa kuripoti kwa wakati klabuni hapo bila sababu za msingi.


“Hao wachezaji wa kigeni wanasajiliwa ili watupe sisi changamoto lakini hatujaiona bado, viwango vyao havitofautiani sana na wazawa na wengine tumekuwa tukiwaacha mbali, uwezo wao umekuwa wa kawaida sana.


“Pili wachezaji hao wamekuwa na nidhamu mbovu sana, wamegeuka mizigo kwenye timu zao, angalia tu jinsi Simba na Yanga zinavyoteseka kuwadhibiti hao wachezaji. Kwa kifupi sijaona umuhimu wao hapa nchini.” alisema Nonga na kuongeza.


“Kwa sasa Kipre Tchetche ndiye mchezaji wa kigeni ambaye naweza kusema ameonyesha kiwango cha kustahili nafasi hiyo pia amekuwa na nidhamu safi ndani na hata nje ya uwanja, tungeanzia kwa wachezaji wa kiwango hicho na siyo hao wengine.


“Nadhani TFF (Shirikisho la Soka Tanzania), ingefanya maamuzi magumu kwa kubana viwango vya wachezaji wanaokuja kucheza hapa nchini, timu zibanwe kusajili wachezaji wenye uwezo wa juu.
”CREDIT:MWANASPOTI

No comments: