ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, July 27, 2014

WANADMV TUPO PAMOJA



WanaDMV Tuko Pamoja !.
Ndugu zangu wanaDMV, nilikuja kwenu rasmi nikiomba kura zenu.Nia yangu ikiwa ni kuungana nanyi katika kutafuta njia za kutatua changamoto zinazotukabili hapa ugenini.
Malengo niliyo nayo kwa jumuiya hii na kwa jamii kwa ujumla sio malengo ya mpito.
Sisi wanaDiaspora  tumeaacha nchi yetu nzuri, wazazi,watoto, ndugu hata marafiki  kwa nia ya kuja kutafuta ahueni ya maisha.Maumivu na changamoto za ugenini ni sababu tosha za kutoruhusu jambo lolote kupotosha malengo yetu.

Nipo pamoja nanyi  kama mgombea asiyefungamana na upande wowote, na nitaendelea kuwa nanyi licha ya matokeo ya Uchaguzi wa Viongozi wa Jumuiya  ya WaTanzania, District of Columbia, Maryland and Virginia  2014.



Asanteni sana.
Harriet Shangarai

No comments: