Advertisements

Friday, August 1, 2014

Magari bila ya dereva kuruhusiwa Uingereza

Serikali ya Uingereza imetangaza kuwa itaziruhusu gari zisizokuwa na madereva barabarani ifikapo mwezi Januari mwakani.

Serikali hiyo pia imetoa wito miji ya Uingereza zitoe mapendekezo ya kuwania kuwa wenyeji wa moja kati ya majaribio 3 ya magari hayo.


Aidha waziri huyo ameagiza kufanywe mabadiliko ya sheria za barabarani ilikuafikiana na mabadiliko hayo ya teknolojia.

Wizara ya usafiri wa umma nchini Uingereza ilikuwa imeahidi kuruhusu majaribio ya magari hayo mwisho wa mwaka uliopita.

Katibu wa Biashara Vince Cable aliyasema hayo katika hafla ya uzinduzi katika kiwanda cha kutengeneza magari cha Mira,kilichoko Midlands.

"tangazo hili la leo linatoa ithibati kuwa magari pasi na madereva yatakuwa barabarani katika miezi 6 zijazo''.

Waandisi nchini Uingereza wakishirikiana na wanavyuoni kutoka chuo kikuu cha Oxford wamekuwa wakifanya majaribio ya matumizi ya magari hayo yasiyo na madereva.

Wadau hata hivyo wamekuwa wakiibua tahadhari ya maswala ya Bima,na uhalali wa magari pasi na madereva jambo ambalo limewalazimu kutumia barabra za kibinafsi kwa majaribio yao.

''Mimi mwenyewe nilijiskia kuwa salama ndani ya gari hilo lililokuwa bila dereva''alisema bwana Cable.

Wakati huohuo Magari hayo yameruhusiwa kufanyiwa majaribio huko Marekani katika majimbo ya California, Nevada na Florida.

Gari linalonadiwa na kampuni ya mtandao wa Google tayari limetumika kwa zaidi ya kilomita laki tatu hivi katika mabarabara ya umma.

Mwaka uliopita kampuni ya 2013 ilifanya majaribio ya gari lake huko Japan.

Barani Uropa kampuni ya kutengeza magari ya Volvo tayari imepata ithibati ya kujaribu magari yake mjini

Gothenburg Sweden.

BBC

No comments: