Mhe. Mwigulu Nchemba Naibu Waziri wa Fedha (S)
Na Nassoro Basalama
Watanzania wana diaspora wanaoishi marekani wameguswa sana na mwigilu, husasan katika kipindi ambacho walipopata fursa ya kukutana naye na kujadiliana juu ya mwelekeo wa taifa letu la Tanzania. Ameonyesha uzalendo, na umakinifu wa hali ya juu katika utambuzi wake wa kazi aliyokuwa nayo kama mbunge na zaidi kama waziri. Watanzania wamejenga matumaini makubwa juu ya tabia yake ya umakinifu wa kusikiliza watu, na kuheshimu mitazamo mbadala ya watoa hoja.
Wana diaspora wanaamini kama Mhe.Mwigilu akikubali kuitikia mwito wa wengi katika kuingia kwenye kinyang'anyiro hiki, taifa hili litapata matumaini makubwa sana ya kiuchumi ambayo ndio kikwamuzi kikubwa cha kiuchumi.
Hii ni dalili nzuri sana ya kupata kiongozi bora. Ukizingati wengine wote wamekuwa wakijipendekeza wenyewe katika kugombania nafasi ya uraisi wa mwaka 2015, lakini tofauti na Mwigilu, ni kijana ambaye, watanzania wenyewe ndio wanaomtaka agombania.
Hususan ukiangalia ni kijana mwenye historia isiyo na dosari.
Vijana wanadiaspora waishio marekani wameshajiandaa kumpeleka Ikulu Mhe.Mwigulu, wanasubiri muitikio wake tu.
Ni magumaini yetu CCM italiona hili na kulizingatia kwa manufaa ya CCM na zaidi kwa taifa letu linalohitaji mwamko zaidi wa kiuchumi na ajira kwa vijana.
9 comments:
Vigezo gani alivonavo kuwa raisi Tanzania. Kelele nyingi he doe not make any sense..kama akiwa raisi Tz ni 10 steps backward.
Tafadhali hebu acheni kutafuta misifa na isikyokuwa na maana kwa kisingizio cha diaspora wamarekani.
Ni lini tumekaa na kukubalina kuhusu hili?
Hivi ndugu zangu watz mkoje? Jamani mnakera sana.
Huyu Mwigulu nani kasema anafaa au ndio keshawalisha mshiko?
STOP THE NONESENSE!!!
Basalama, if you trained as a journalist, obviously, your journalism teachers sent you off prematurely. You need to go back to school. If you are not a journalist, you should stay out of that field, because you do not have the potential to attain even some sort of amateurish proficiency in journalism. Otherwise, if you claim to be publishing views of others, be sure to support such publication with emperical data. Period.
Nasoro, kwa kiingereza cha kimarekani, ulichokifanya kinaitwa "brown nosing"
Kwa kifupi tu tuacheni kupiga debe zisizofaa, huyu baaado kabisa na wala wana DMV au wakazi wa Marekani hatujaona alilofanya zaidi k ya kubeza vyama bya upinzani navyo ni vyama. Kazi aliyoepewa hajaonyesha utendaji wake kabisa yeye na siasa tu hatuna neon ila Uraisi baado sana na hatauweza tusiipeleke nchi kusiko jamani.
Lilikuwa kuwa la msingi, whether Mwigulu Mchemba is the best choice for the position or not, mtoa mada hakuwa sahihi kuongelea maoni yake km ya diaspora kwakuwa hakuna concensus kuhusiana na hili.
Hawa wanaoandika ni kwa niaba ya nani???????
Nassoro Bsalama - you don't speak for wana-diaspora, you speak for yourself.
Raisi Tanzania ni Lowasa wengine wanapiga kelele tu
Post a Comment