Advertisements

Friday, August 1, 2014

MARAIS WASTAAFU THABO MBEKI, FESTUS MOGAE NA BENJAMIN MKAPA WAKUTANA DAR ES SALAAM‏

Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini na Festus Mogae wa Botswana wakiigia kwenye chumba cha Mkutano katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo wakati wa mkutano wa mwaka wa African Leadership Forum ulioandaliwa na Taasisi ya Uongozi Institute jijini Dar es salaam ambao ulikuwa unajadili changamoto mbalimbali zinazozikabili nchi za Afrika na kuangalia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na hatua za kushughulikia changamoto hizo.
Rais mstaafu wa wa Afrika Kusin Thabo Mbeki akizungumza katika mkutano huo uliojumuisha viongozi mbalimbali wa afrika na taasisi mbalimbali kweye hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo.
Marais wastaafu Thabo Mbeki wa Afrika Kusini katikati ,Festus Mogae wa Botswana kushoo na Rais Mstaafu wa Tanzania Mh. Benjamin William Mkapa wakiwa wakiongoza mkutano huo.
Baadhi ya viongozi kutoka taasisi mbalimbali waliohudhuria katika mkutano huo.
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Mh. Zitto Kabwe (katikati) ni mmoja wa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Fredrick Sumaye(kulia) na Mh. Balozi Ali Karume walikuwa ni miogoni mwa viongozi waliohudhuria katika mkutano huo pia.

No comments: