Advertisements

Wednesday, December 24, 2014

DIAMOND AANIKA SABABU 5 ZA KUMPENDA ZARI, ACHAMBUA UBOVU WA WEMA, PENNY NA JOKATE

Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akiwa na mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady.
Mapenzi bhana! Baada ya kutoka kimalavu na kumwagana na mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’ kisha kuangukia kwenye ‘utamu’ wa penzi la mwanamama anayekimbiza Uganda, Zarinah Hassan a.k.a Zari au The Boss Lady, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ameamua kuanika siri tano za kilichomvutia kwa staa huyo gumzo Afrika Mashariki.
Akizungumza katika mahojiano maalum katika ofisi za gazeti hili, Bamaga-Mwenge jijini Dar hivi karibuni, bila kupepesa macho au kuuma maneno baada ya kuulizwa kinagaubaga juu ya ukaribu wake na Zari, Diamond au Dangote hakutaka kuficha, akaamua kuweka mambo yote hadharani.
MATANGAZO
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa na mwenye heshima, wakati mwingine natakiwa kuwa na akili ya kuwa na uhusiano na watu ambao watakuwa msaada kwangu pia.
“Siwezi kuwa karibu na mtu ambaye hataniongezea kitu chochote kile. Baada ya kujitangaza sana Tanzania, nikahamia Kenya ambapo nilikuwa karibu na mwanadada Avril. Ukaribu wangu kwake, ukanifanya Kenya kutambulika.
“Baada ya kukaa kwa muda, nikataka nitambulike na Uganda pia, unafikiri ningefanya nini? Nikaliteka soko lao kwa kuwa karibu na mrembo Zari.
“Kweli nimefanikiwa na hata siku ya shoo yake (Desemba 18, mwaka huu nchini Uganda), ilikuwa ni balaa kiasi kwamba sikuamini kilichokuwa kimetokea, watu walikuwa nyomi ile mbaya. Mbali na kuwa mwanamuziki mkubwa, bado nahitaji kujitangaza zaidi.”
Zari na Diamondi wakibusiana kimahaba.
MSISIMKO
Sababu ya pili aliyoitaja ni kwamba Zari ambaye ni mama wa watoto watatu ana msisimko wa aina yake tofauti na ‘mashori’ wengine aliwaowahi kuanguka nao dhambini.
“Hakuna mwanaume anayependa kukaa na msichana asiyekuwa na msisimko wa kimapenzi. Hebu fikiria umekaa na mwanamke mwenye umbo kama la mwanaume, utapata msisimko gani hapo? Lakini mcheki mtoto alivyong’aa, anameremeta, mtoto yupo bomba, ukikaa karibu yake tu utagundua kwamba umekaa na msichana mwenye mvuto ambaye kila wakati atakufanya kuwa bize kumwangalia.”
BIASHARA
Sababu ya tatu aliyoitaja Diamond ni kwamba mwanadada huyo yupo vizuri kibiashara.
“Ninaangalia fedha, ili biashara zangu ziweze kupiga hatua sina budi kukaa karibu na mfanyabiashara mwenzangu (Zari) kwa ajili ya kushauriana biashara ziende vipi. 
“Yeye (Zari) ni mkongwe katika biashara, kuwa karibu naye naamini nitajifunza mambo mengi sana.
Amekuwa muwazi kwangu na amenipa mianya mingi ya kufanya biashara, lakini je, nisingekuwa karibu naye, michongo hiyo ningeipata vipi?”
Zari na Diamondi wakiwa kwenye pozi.
UZURI
Sababu ya nne ya kuwa na Zari, Diamond alidai kwamba mwanamama huyo ni mzuri kupita maelezo.
Alifunguka: “Mimi ni mwanamuziki mkubwa, watoto wazuri wananipenda kwa hiyo kama ningefanya uamuzi wa kuwa na mwanamke asiyekuwa mzuri, maneno yangeanza kusikikasikika na isingekuwa poa. Mbali na kuwa mfanyabiashara, kumtumia kama msaada wa kunitangaza, lakini Zari ni mzuri bwana. Ni mwanamke ambaye kwa kumwangalia tu, unaweza kusema kwamba haujawahi kukutana na mwanamke mzuri kama yeye.
ANAJITAMBUA
Sababu ya mwisho aliyoianika Diamond ni kwamba Zari yupo vizuri kichwani kwa maana ya kujitambua tofauti na wanawake wote aliowahi kutembea nao.
 
Mwanadada mwenye mvuto Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Beautiful Onyinye’.
“Nimekuwa na wanawake tofautitofauti lakini kwa Zari, ni mwanamke mwenye hekima na anajitambua sana. Si mzungumzaji kivile na huwa anapenda kufanya vitendo kuliko maneno.
“Anajua ni kipi anatakiwa kufanya na akili yake ameielekezea kwenye fedha zaidi. Hapendi masihara na fedha, anapenda kujitoa na ni mchakarikaji sana. Nampenda mwanamke wa hivyo kwa kuamini kwamba atanifanya nijitume zaidi.”
AWACHAMBUA JOKATE, WEMA NA PENNY
Diamond alipoulizwa juu ya kasoro za warembo wakali Bongo aliowahi kutoka nao wakiwemo mrembo Jokate Mwegelo ‘Kidoti’, Wema na mtangazaji wa Radio E-FM, Penniel Mungilwa ‘Penny’, aliwachambua mmoja baada ya mwingine na kuhitimisha kuwa ni wazuri lakini hawamfikii Zari.
Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’.
UTAMBULISHO KESHO DAR LIVE
Mbali na kuziweka wazi sifa za Zari, jamaa huyo alidai kwamba atamtambulisha rasmi kwa Wabongo kesho usiku kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Burudani wa Dar Live, Mbagala jijini Dar atakapokuwa anaangusha burudani ya kibabe katika Tamasha la Wafalme akiwa na mfalme mwenzake, Mzee Yusuf na wakali wengine kibao kwa kiingilio cha shilingi 10,000/= kwa kawaida na shilingi 20,000/= kwa V.I.P.

9 comments:

Anonymous said...

sasa wakina wema na team wema wako wapi,hata kama habari hizi si za kweli lakini mjiulize nyinyi wasichana na mnajifanya wazuri na viteam vyenu,mwenzenu huyu wa mbagala yeye anatafuta mwanya kwenu ili ajitangaze jina na pia kupata pesa kutoka migongo yenu nyinyi wakina mama.
si mlaumu but mkae mkijua mwanamme haji kwenu tu kwa uzuri wenu anakuja kwenu pia kutafuta riziki yake na michongo yake huyu jamaa opportunisms sana kupita maelezo sasa wema yamekutokea kinyogo UKIONA MWENZAKA ANANYOLEWA NA WEWE TIA MAJI KICHWANI,JAMAA ANAKUPANGENI FOLENI TU BILA KUMSHITUKIA MNADHANI PENZI KUMBE MWENZENU ANAYAKE AKILINI.
BIG UP BIG UP BIG UP MTOTO WA MBAGALAAAAAAAAAAAAA.TANDALEEE MANZESEE ETC.

Anonymous said...

This guy English zero, he needs to learn very hard that is a business language. he is lacking wisdom mshamba na limbukeni uwezi kusema hayo kama umestaharabika.

Anonymous said...

He never went to any school, sad story interviews zake, I never understand him

Anonymous said...

Ni kweli kabisa I agree with you ni limbukeni tena saana. Tatizo hana watu wanaomshauri wana mwacha tu anajiropokea. Diamond atakwisha sasa hivi give him only one year. He is everywhere anacolabo na kila mtu hachagui who does that? Atachujika sasa hivi wait and see

Mlay said...

Diamond is a smart business man. He sees opportunity and grabs it! Word up...

Anonymous said...

maneno yako diamond ni kweli 100% kwa nnavyomuona huyu Zari ni mzuri hasa na mapesa anayo, mimi naishi USA kumuona mwafrika wa Uganda tena mwanadada anamiliki Lamborghini, maserati, na range rover, besides nilimuona akifanya mahojiano na Sporah, namvulia kofia na nakupigia salute umepatata kwa sasa hao wapenzi wa zamani hawafikii hapo maji makubwa sana hayo. kama ulivyosema tafuta relationship zenye faida kwako sio wanywa pombe tu bila maarifa. na hawa ma anonymous wanaodhani kuongea kiingereza kingi ndio kuwa smart wamechelewa. majapani wakorea wachina wafaransa na wengineo wana maendeleo vizuri tu bila hata kukitumia hicho kiingereza. good job keep it up brother!!!

Anonymous said...

UKIMFUATA MTU KWENYE PENZI KWA AJILI YA PESA ZAKE AU UMARUFU WAKE UZURI WAKE ZIKISHA UTAFANYAJE?
UTAMKIMBIA?NA UKIMKIMBIA NI LIBUKENI,PESA SI KILA KITU ETI WATU WANAKUJA HAPA NA KUTETEA ETI ANA AMBORGHINI MSERATI RANGE ROVER, YANI AMEKALIA PESA PESA TU NO WONDER ALIZALIWA MASKINI MTU WA NAMNA HII,NDO MIAFRICA TULIVYO NA KUPAYUKA NA VITU KULIKO UTU WA MTU.NA NDO MAANA MNAPIKIGA KISANA

WHAT A SHAME WENZENU WANATAFUTA ELIMU NYINYI MNAKODOLEA MIMACHO MALI ZA WANAWAKE MIJANADUME MIJITU MIZIMA OVYOO NA MIDEVU YENU USONI NA .CHINA

Anonymous said...

maisha ni pesa huo ndo ukweli wewe kama unadhani umasikini ndio mtaji wako basi kaa nao peke yako wenzio sisi mapesa mbelee, muhimu ni ya halali si ya kumkaba wala kumdhulumu mtu. cha msingi tunazidiana ujanja wa kuzipata tu lakini mapesa kwanza ndio sabuna ya roho, ufukara baki nao wewe Anonymous wa december 25 10.03 pm. Diamond na wengine pia hangaikeni kuitafuta pesa kuwa na uhusiano wa karibu na smart people ni muhimu sana faida yake utaiona

Anonymous said...

Mmmhhh, am not team wema or zari bt kaka Yangu diamond kuwa makini na kauli zako. Hizo co kauli nzuri kwa ma ex wako.