Advertisements

Wednesday, December 24, 2014

MAZITO NA MAPYA YAIBUKA BAADA YA SHILOLE KUVALISHWA PETE YA UCHUMBA, UMRI NA MICHEPUKO VYAHUSIKA

Chichi Baby akiwa na Baiby baibyyyyyy!!
Mara tu baada ya mwanadada mwaigizaji wa filamu na mtafutaji kunako tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Zuwena Mohammed ‘Shilole’, kuvalishwa pete ya uchumba na mchumba wake, Naftari Mlawa ‘Nuhu Mziwanda’ tayari watu wameanza kuisengenya.
Shilole alivalishwa pete hiyo katika sherehe yake ya kuzaliwa iliyofanyika katika ‘apartment’ za Baraka Plaza, Mikocheni jijini Dar ambapo mara baada ya mwanadada huyo kukata keki na kuwalisha watu mbalimbali waliohudhuria, ndipo Nuhu alipomsapraizi mwanadada Shilole kwa kumvisha pete hiyo.
Kitendo hicho kilionekana kukubalika na waalikwa wengi, lakini wengine hawakufurahishwa nacho kwa madai eti kwamba Nuhu ni mdogo kuliko Shilole hivyo hakustahili kuvisha pete mtu mwenye umri kama dada’ke.
“Mh! Mwenzangu hii kali, mimi siku zote Nuhu niliamini hayupo serious kutembea na Shilole maana ni mkubwa kuliko yeye lakini sasa hapa kanishangaza kweli, kwa nini asitafute mdogo mwenzake?,” alisikika dada mmoja ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake.
Hata hivyo licha ya masengenyo hayo kusambaa chini kwa chini, Nuhu aliwakata watu vilimilimi kwa kutamka hadharani kuwa wanapendana na Shilole hivyo haoni ajabu kama kuna watu hawatakubaliana na penzi lao.
“Tukio linalotendeka hapa limepewa baraka zote na wazazi wetu wameridhia mimi na mchumba wangu tuoane na hii ni hatua ya kwanza tu mengine yatafuata na msishangae sana kuona wazazi wetu hawapo eneo hili ni kwamba wanatambua kinachoendelea hapa.
“Najua wengi mtakuwa na maswali kuhusu hili, mimi na yeye tunapendana na ndiyo maana leo hii namvisha pete mpenzi wangu na Mungu atatujaalia katika maisha yetu,” alisema Nuhu na sherehe ikaendelea kwa watu kula na kunywa.
Sherehe hiyo ilihudhuriwa na mastaa mbalimbali akiwemo Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Wellu Sengo ‘Matilda’, Shettah, Martin Kadinda, Mh. Temba, Chegge, DJ Choka na DJ Tass.
Steve Nyerere aliyekuwa MC wa shughuli hiyo alisema Shilole ni shemeji yake kwani yeye ni kaka yake Nuhu, na kwamba tukio linalofanyika hapo, wao kama ndugu wamekubaliana na ndoa itafungwa.
“Siku zote huwa namwambia shemeji yangu kuwa yeye ni mtafutaji kwa hatua aliyofikia mpaka sasa na ninamkubalisana shemeji yangu, karibu Iringa,” alisema muongoza sherehe huyo.

3 comments:

Anonymous said...

yani udaku mwanzo mwisho sasa ndo iweje unavishwa pete leo kesho unabwagwa yasije yakawa ya wema septum hamjambui mnaambiwa mnakaa kujiremba remba na ubisho njiwaa.

yani hata hamjui kuwasoma wanaume maasa ya nyakati.

tunasubiri ndoa na muishi mje mzikane hapo ndo tutajua kweli mlipendana kikweli kweli si eti leo kututambia na kuvishwa pete.

wasichana hawa wajinga sana

Mlay said...

Waache

Anonymous said...

we mlay kazi yako kutetea ujinga sana waache angekuwa ndugu yako wa kike ungependa mambo haya kipuzi puzi ayatende.