Advertisements

Wednesday, December 24, 2014

Mkwasa: Yanga tembeeni kifua mbele.

Kocha msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa.

Kocha msaidizi wa Yanga, Boniface Mkwasa amewataka mashabiki wao kutembea kifua mbele kwa kuwa mafanikio yanakuja.
Katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ofisi za makao makuu ya Yanga jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya klabu hiyo, Jerry Muro alisema Mkwasa amemhakikisha kikosi chao kiko vizuri kambini mjini Bagamoyo, Pwani kujiandaa kwa mechi inayofuata dhidi ya Azam FC.

"Tumewasiliana na kocha msaidizi (Mkwasa) leo (jana) asubuhi. Ametuambia kikosi kiko vizuri na hakina mchezaji hata mmoja aliye majeruhi. 
Amewataka wanayanga sasa kutembea kifua mbele maana mambo mazuri yanakuja," alisema Muro.

Katika hatua nyingine, Katibu Mkuu mpya wa Yanga, Jonas Tiboroha, aliyekuwa amefuatana na Muro jana, alisema anataka kuiongoza klabu hiyo kujiendesha kiuchumi badala ya kutegemea ufadhili.

Tiboroha alisema katika mpango wake huo, anataka kuanza kutengeneza kikosi imara cha ushindani ikiwa ni pamoja na kutengeneza mifumo bora ya soka la vijana klabuni hapo.

Tayari uongozi huo mpya wa Yanga umeshaweka wazi kwamba umedhamiria kushinda mechi tatu zijazo za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Azam FC, Mbeya City na Coastal Union.
CREDIT:NIPASHE

No comments: