Advertisements

Thursday, December 25, 2014

Usiku wa Black &White 55th Birthday Bash ya Asia Idarous Khamsin wafana

NA ANDREW CHALE
SHEREHE maalum ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 55 ya kuzaliwa kwa Mama wa Mitindo, Asia Idarous Khamsin ‘Black &White 55th Birthday Bash’ usiku wa Desemba 24 ulifana huku Spice Modern Taarab wakikonga nyoyo wadau mbalimbali waliojitokeza ndani ya M.O.G Bar (Zamani Nyumbani Lounge) katika tafrija hiyo.
Sherehe hizo zilizoandaliwa na Wabunifu wa mavazi wachanga na wanaochipukia nchini, uliojulikana kama ‘Black &White 55th Birthday Bash Asia Idarous Khamsin’ ambapo wadau mbalimbali walipata wasaha wa kujumuika pamoja sambamba na burudani hiyo ya Spice Modern taarab.
Kwa upande wake, Asia Idarous Khamsin alimshukuru Mungu kwa mema anayomtendea hadi kufikisha miaka 55, ambapo aliitaka jamii kuendelea kusimamia mema ikiwemo matendo yampendezayo Mwenyezi Mungu.
Aidha, wadau mbalimbali walijitokeza kwenye tafrija hiyo, wakiwemo wabunifu, wasanii na watu maarufu. Wakiwemo wabunifu Rio Paul, Martin Kadinda, Faustian Simon na wengine wengi ambao wanachipukia kwa sasa kwenye tasnia hiyo.

Pichani ni Picha za tukio hilo jana usiku wa: Black &White 55th Birthday Bash
Asia Idarous akiwa na wadau waliojitokeza kujumuika naye.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi

No comments: