Muonekano wa sasa katika hatua za awali za ujenzi wa barabara ya Mbezi mwisho-Goba-Tangibovu eneo la Goba
Mbunge wa Jimbo la Ubungo, John Mnyika akizungumza na Waziri wa Ujenzi, Dkt. Pombe Magufuli
Barabara nyingine ni ile ya External-Kilungure hadi Kimara Korogwe kilometa 8.0, Wazo Hill-Goba hadi Mbezi Mwisho kilometa 20 na Goba-Tangi bovu kilometa 9.0
Waziri Magufuli alisema, barabara ya Wazo Hill-Goba yenye urefu wa kilometa 20 ikikamilika kwa kiwango cha lami itaziunganisha barabara za Bagamoyo na Morogoro ambazo zimekuwa zikikabiliwa na msongamano kwa muda mrefu.
Pia, barabara ya Kinyerezi-Kifuru hadi Mbezi Mwisho yenye urefu wa kilometa 14 itapunguza msongamano kwa kiasi kikubwa kwa kuwa itakuwa inaunganisha barabara ya Morogoro na Nyerere.
Kwa umuhimu sana, Waziri Magufuli alisisitiza; "kumbukeni mkiiba vifaa vya ujenzi hamuibi vifaa vya kampuni zinazojenga bali mnajiibia wenyewe kwa sababu hizi ni fedha za kodi ya wananchi bali kwa kufanya kazi kwa bidii na uadilifu kutawezesha ujenzi wa barabara kukamilika kwa wakati na ninyi (mafundi) kujihakikishia uhakika wa ajira."
Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini (TANROADS), Eng.Patrick Mfugale ameiomba serikali kuongeza bajeti ya barabara ili kuwezesha miradi ya barabara kukamilika kwa wakati na kuwataka wananchi kutoa ushirikiano kwa wakandarasi ili barabara zijengwe kwa kiwango kilichokubalika katika mikataba.
1 comment:
hIZI TYPE ZA BARABARA HAZIDUMU, MVUA IKINYESHA TU TATIZO, HELA MMECHEKECHUA.
Post a Comment