kiatu cha asili kilichotengenezwa kwa udongo ambacho kinauzwa kati ya Tsh 160,000 kwa kimoja na pea moja ni Tsh 320,000 kiatu hiki ni moja kati ya vivutio vya utalii katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa vinavyotengenezwa eneo la Rungemba na kuvutia watalii wa ndani na nje
Baadhi ya vifaa mbali mbali vilivyotengenezwa kwa udongo eneo la Rungemba Mufindi ni zaidi ya utalii.
Majiko na vyungu vilivyotengenezwa kwa udongo
Mmoja kati ya wanahabari mkoani Iringa Mawazo Marembeka akitazama vyungu eneo la Rungemba Mufindi mkoani Iringa
Afisa utalii kanda ya kusini Tanapa Bi Risala Kabongo (kushoto) akitazama vyungu na dhana mbali mbali za kitalii eneo la Rungemba
Kiatu kilichotengenezwa kitalii zaidi kwa udongo.
VYUNGU vya asili vinavyotengenezwa kijiji cha Rungemba katika wilaya ya Mufindi mkoani Iringa vinaweza kusaidia kuitangaza wilaya ya Mufindi kiutalii zaidi iwapo serikali ya wilaya hiyo itawawezesha na kuwahamasisha zaidi wananchi wilayani humo kujiajili wenyewe katika ufinyanzi.
Kijiji hicho cha Rungemba ambacho kwa sasa wananchi wake hasa wanawake wameendelea kujipatia kipato zaidi kutokana na ufinyanzi wa vyungu na mapambo mbali mbali yatokanayo na ufinyanzi ,kimeendelea kujipatia wageni zaidi wa ndani na nje ambao wamekuwa wakifika kupata huduma ya kazi itokanayo na ufinyanzi.
Akizungumza na mmoja kati ya wanawake wanaojishughulisha na ufinyanzi wa vyungu eneo hilo Bi Anna Kalinga alisema kuwa awali walianzisha eneo hilo kama utani utani ila kwa sasa eneo hilo limeendelea kupata umaarufu mkubwa na hata gharama za vyungu na mapambo mengine imeendelea kukua zaidi.
Hata hivyo alisema kuwa idadi ya wananchi kupenda kutengeneza vitu vya utalii kwa kutumia udongo imeendelea kuongezeka huku baadhi ya watu wameanza kuboresha maisha yao kwa kujenga nyumba za kisasa na kusomesha watoto kupitia kazi za ubunifu wa kitalii.
Alisema katika eneo hilo wanatengeneza vitu mbali mbali za kitalii vikiwemo vitu mfano wa viatu vya kupandia maua ambavyo gharama yake ni kati ya 160,000 hadi 320,000 kwa viatu viwili kwa maana ya pea moja huku vyungu vimekuwa vikiuzwa kati ya shilingi 45,000 hadi 75,000 na kuwa bei hiyo imepandishwa kutokana na ongezeko la watalii katika eneo hilo .
" Eneo hili kwa sasa limeendelea kuwa maarufu sana kwa kutangaza utalii na utamaduni wa kitanzania kupitia ufinyanzi ila bado serikali haijatambua na kuelekeza nguvu zake zaidi eneo hilo kwa kuweka utaratibu mzuri wa kuvutia watalii kufika hapa"
Mkuu wa wilaya ya Mufindi Evarista Kalalu akizungumzia utalii wa eneo hilo alisema wilaya yake ilianza mchakato wa kubainisha vivutio vya utalii pamoja na kukusudia kushirikiana na familia ya Chifu Mwinyigumba ili kuweka mazingira mazuri eneo la makaburi kama sehemu ya historia pindi watalii wanapofika kutembelea eneo hilo.
Wakati kwa upande wa wasanii hao wanaotangaza wilaya kupitia ufinyanzi za vitu mbali mbali za utalii alisema ofisi yake ilianza mwaka 2007 kwa kuwapeleka baadhi ya wana kikundi Kyela mkoani Mbeya kujifunza namna ya utengenezaji wa vyungu bora na dhana nyingine ili kuvutia watali zaidi japo kwa sasa wilaya hiyo haina afisa utalii baada ya aliyekuwepo kufariki dunia mwaka jana .
Afisa utalii kanda ya kusini Tanapa Bi Risala Kabongo alisema kuwa eneo hilo la Rungemba ni moja kati ya maeneo ya vivutio vya utalii katika mikoa ya kusini na kuwa wilaya ya Mufindi pamoja na vivutio vingine bado wanapaswa kuboresha eneo hilo ili kulitumia kama sehemu ya utalii na kuwa suala la utalii linajumhisha mambo mbali mbali yakiwemo ya hoteli ,biashara na wanyama ,maji ,tamaduni ,na mambo mengine mengi ambayo wageni hupenda kujif
No comments:
Post a Comment