Advertisements

Saturday, February 28, 2015

RUFAA YA CHEKA KUSIKILIZWA DAR-ES-SALAAM FAILI LA KESI YAKE KUTUA SIKU YEYOTE

Baba wa Francis Cheka akiwa na majonzi baada ya mtoto wake kuhukumiwa kwenda magereza miaka mitatu.
Mkakati wa kumkatia rufaa bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Francis Cheka, bado unaendelea ambapo kwa sasa faili la hukumu ya kesi yake linatarajia kutua jijini Dar katika Mahakama ya Rufaa siku yoyote.
Cheka anatumikia kifungo cha miaka mitatu baada ya kupatikana na hatia ya shambulio la kudhuru mwili dhidi ya meneja wa baa yake, Bahati Kibanda, lililofanyika Julai 2, mwaka jana.

Mmoja wa memba wa familia ya Cheka amesema mchakato wa kumkatia rufaa unaendelea vizuri ambapo muda wowote faili la hukumu ya kesi yake litawasili jijini Dar.


“Kwa upande wetu mchakato wa rufaa tumeukamilisha ambapo kwa sasa kilichobaki ni faili la hukumu ya kesi yake kutua jijini Dar katika Mahakama ya Rufaa.

“Mwanasheria aliyeteuliwa tayari ameshatueleza kuwa tusiwe na wasiwasi, zaidi ni kumuomba Mungu ili kila kitu kiende sawa, kwa maana hiyo lazima Cheka atahamishiwa jijini humo kwa ajili ya kuisikiliza tena rufaa ya kesi yake,” kilieleza chanzo hicho.

1 comment:

Anonymous said...

Hii Habari ina kasoro za kiufundi. Hakuna kesi inayoweza kutoka mahakama ya Hakimu Mkazi kwenda Mahakama ya Rufaa bila kwanza kuwa imesikilizwa na Mahakama Kuu.