Advertisements

Saturday, February 28, 2015

Simba yatakata, yaichapa Prisons 5-O, Ajib atupia hat-trick

Na Richard Bakana, Dar es salaam

Klabu ya Simba ya Jijini Dar es salaam leo imefanikiwa kutoa dozi ya msimu kwa maafande wa Tanzania Prisons, baada ya kuwafunga mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania bara uliopigwa katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.

Katika mchezo huo mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib ndio aliibuka kinara wa kufumania nyavu baada ya kutupia kambani bao 3 (Hat trick) ambapo katika kipindi cha pili alipumzishwa baada ya kupewaa kadi njano.

Simba walijipatia ushindi huo kupitia kwa Ibrahim Ajib dakika ya 15, dakika 21 na dakika ya 42 kwa mkwaju wa penati, na kufanya muamuzi wa mchezo huo Odongo ampatie mpira wake kwa kazi nzuri aliyoifanya.

Baada ya kutengeneza nafasi nyingi za mabao Okwi naye akaiandikia Simba bao la nne katika dakika ya 74 kabla ya Ramadhan Singano kumaliza kazi kwa kufunga bao la tano katika dakika ya 82 kufatia kazi nzuri ya Emanuel Okwi.

Kwa ushindi huo Simba inakuwa imeweka rekodi nzuri ya kufunga mabao mengi katika mchezo huku ikiwa ni salamu kuelekea mchezo na Yanga wiki kesho Machi 8.
CREDIT:SHAFFIHDAUDA

No comments: