Advertisements

Friday, March 6, 2015

Rais Kikwete Azindua AZAMTV



Rais Jakaya Kikwete amekuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa studio ya kisasa ya Azam Tv itakayojulikana kama Uhai Production iliyopo eneo la Tabata kando ya barabara ya Mandela.

Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam Media, Tido Mhando amesema studio hiyo ni ya kisasa na haifanani na studio yoyote ya chombo chochote cha habari hapa Tanzania. Aidha alisema hadi kukamilika kwa ujenzi wa studio hiyo, zaidi ya dola za kimarekani milioni 31 zimetumika.
Mkurugenzi wa Uendeshaji, Yahya Mohamed amesema hadi kukamilika kwa ujenzi wote, kutakuwa na studio tatu. Hadi sasa, ni moja tu ndiyo iliyokamilika.

No comments: