Wakazi wa Mloganzila wa Kata ya
Kwembe wilayani Kinondoni wakiwa katika Ofisi ya Wizara ya
Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ajili kudai fidia maeneo yalichukuliwa
katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya
Kufatilia Madai kwa Wakazi wa Mloganzila –Kwembe,Fedrick
Schone akitoa malalamiko yao katika Ofisi za wizara ya Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushoto ni Naibu
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angela Kairuki akisikiliza madai
ya wananchi wao leo jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ardhi,Nyumba
na Maendeleo ya Makazi ,Angela Kairuki akizungumza na baadhi ya wananchi katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi juu ya wananchi walioenda kudai fidia za maeneo yalichukuliwa
katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam leo. (PICHA
ZOTE NA EMMANUEL MASSAKA)
Na Chalila Kibuda
WAKAZI wa Mloganzila wa Kata ya Kwembe wilayani Kinondoni leo
wameandamana katika Ofisi ya Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa
ajili kudai fidia maeneo yalichukuliwa katika Mradi wa Hospitali ya Taifa ya
Muhimbili,jijini Dar es Salaam.
Kuandamana huko kumetokana na serikali
kuchelewa kutoa majibu juu ya fidia ya ardhi pamoja na mapunjo ya fidia
yaliyotokana na nyumba ,mashamba katika eneo hilo lililochukuwa na mradi
huo.
Maandamano yalikuwa ya aina yake
kutokana na kuwa na misafara ya magari matatu na kuingia mmoja moja na kisha
kujaa katika mlango mkuu wa wizara hiyo na kuanza kupiga kelele kwa kile
walichodai hatima yao ya kulipwa ili waendelee na maisha yao.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kufatilia
Madai kwa Wakazi wa Mloganzila –Kwembe ,Fedrick Schone kufika
kwa wanachi katika ofisi ni katokana na kuwepo kwa kalenda nyingi zisisotoa
suluhu ya mgogoro wao wa madai.
Amesema kamati yao imekosa
kuaminika kutokana na kupeleka majibu ambayo yamekuwa yakiibua maswali mengi
kwa wananchi waliochuliwa maeneo yao.
Akizungumza wananchi hao,Naibu
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ,Angela Kairuki amesema madai yao
watashughulikia ndani ya siku saba kwa kwenda kuzungumza na wananchi hao baada
ya kujadili na Waziri wake.
Amesema kuwa suala hilo limefika na
kudai anawapa barua juu ya utekelezaji ndani katika kuweza kufikia suluhu na
kuwataka kuondoa wasisi wa jambo hilo.
No comments:
Post a Comment