Advertisements

Friday, May 1, 2015

Tuache ushabiki Jamani Huyu Dada Tumpe Hongera yake... Ubunifu Wake Nimeupenda..Mitandao ya Kijamii leo ni Zari Zari


Zari "Watanzania Wamenikaribisha kama ni mtu wao na sasa mimi ni wao hivyo ni yote ni heri kabisa"

Zari Tlale aka The Bosslady amesema upendo anaoupata baada ya kuanzisha uhusiano na Diamond Platnumz, umemfanya agundue kuwa watanzania wamemkubali kama mtu wao.

Akiongea na Clouds FM/TV asubuhi hii, Zari amesema tangu ameanza kuja Tanzania amekuwa akipokea upendo zaidi kutoka kwa watanzania kiasi ambacho kimemfanya ajisikie kama yupo kwao.
“Siwezi hata kulalamika, watu wa Tanzania ni wakarimu sana ni watu wazuri sana, kwangu mimi sijapata hata tatizo, siwezi hata kusema kitu chochote kibaya kuhusu watu wa Tanzania,” alisema.

“Wamenikaribisha kama ni mtu wao na sasa mimi ni wao hivyo ni yote ni heri kabisa,” aliongeza.

Katika hatua nyingine Zari amesema Tanzania itageuka kuwa makazi yake ya mara kwa mara na mipango iliyopo ni kuanzisha mradi wa kibiashara nchini lakini baada ya kufanya utafiti na kubaini fursa za uhakika.

“Siwezi tu nikafungua biashara hapa eti kwasababu mimi ni maarufu nikafungua tu biashara ya kijinga na nikidhani ninaweza nikauza wazo langu la kijinga kwa watu hapa, wao sio wajinga wanatumia hela zao hivyo nahitaji kubaini wapi kuna hitaji, kipi naweza kufanya na hapo ndipo ntaenda na kuwekeza fedha zangu.”
Mrekebisha Tabia Ameandika Hivi:
Huyu dada nimempend a mnoo!! Kwenye suala la kutafuta pesa...tumpe hongera yake! Ubunifu nimeupenda...Akipata fursa anaitumia kisawasawa...Zari White Party ni idea yake na alivyoshirikiana na management ya Diamond imekuwa tamu sana, itakuwa wametoa pesa nyingi sana kuandaa lkn wameingiza pesa nyingi pia maana wamepata wadhamini wa kutosha...hapo hata wakigawa baadhi ya tickets bure sion shida kuhusu hili.

Hapa nataman na mastaa wetu waige mfano au wamzidi kwa kufanya kitu cha maana na cha maendeleo....inawezekana!!! Tatizo langu ni moja tu!! Why mtu umtukane mtanzania mwenzako na kuunda magroup ya kudhalilisha eti kisa ni Zari...hatuwezi kumsapoti mtu mpaka mwingine atukanwe kwanza?

Watanzania tuacheni hizo, tunazidiwa na watu wa nchi nyingine. Sijui nani katuroga!!!


Patrick Gondwe Ameandika Hivi :

"Zari:huyu mdada kupitia perceptions za media nilikuwa nikiamini ni chakaramu tu kama akina ...... lkn baada ya interview nimekuwa na mtazamo tofauti.... kumbe huyu ndie aliemfaa diamond haswaa.... kichwani ni 3D huyu.... namna anavyozungumzia investments pengine ndilo lilikuwa jawabu kubwa alilokuwa akilitafuta mtoto wa mbagala.... tena huyu alipaswa kuwa meneja wake kabisa"

My Take.......

She is really a lady Boss.....Proved....

No comments: