Advertisements

Sunday, August 2, 2015

Hii ndio Historia na Asili ya Mji wa Tanga.???

Mji wa Tanga ni Mji Mkuu wa Mkoa wa Tanga uliopo ufukweni mwa Bahari ya Hindi. Tanga ina bandari kubwa kabisa katika sehemu ya kaskazini mwa Tanzania. Njia ya reli kwenda Mji wa Moshi inaanza hapa.

Jina hili la mji wa Tanga lilitokana neno la Kiajemi lenye maana nne tofauti ambazo ni: Iliyo nyooka; 
Bonde lenye rutuba; 
Barabara upande wa mto na 
Shamba juu ya mlima.
Neno hilohilo la Tanga kwa kabila la Kibondei ambalo ni wenyeji wa mkoa huo lina maana ya shamba, wao hulitamka N'tanga.

Tanga insaemekana imeanzishwa na wafanyabiashara Waajemi katika karne ya 14 KK. Mji wa Tanga haukupata umuhimu kama mji wa jirani ya Mombasa. Tarihi ya Pate inasema ya kwamba kabla ya kuja kwa Wareno., Pia Pate iliwahi kutawala Lindi kwa muda fulani.

Katika karne ya 19 KK, Tanga ilikuwa chini ya utawala wa Omani na Zanzibar. Misafara ya biashara imeanzishwa hapa kwenda bara. Kutokana na bandari yake nzuri ya kiasili Tanga ilikua sana wakati wa ukoloni wa Wajerumani waliojenga bandari ya kisasa pamoja na reli kwenda Moshi. Reli iliwezesha kilimo kwa ajili ya soko la dunia na Tanga ikawa bandari kuu kwa ajili ya katani na kahawa. Baada ya Uingereza kuchukua utawala wa Afrika ya Mashariki ya Kijerumani, reli ya Tanga-Moshi iliunganishwa na ile ya kati hivyo ikawa na njia kwenda Daressalaam pia. 
Wakati wa Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia Tanga iliona mapigano makali tar. 3 - 5 Novemba 1914. Jaribio la Uingereza kuvamia Tanga kwa kikosi cha maaskari 8000 Waingereza na Wahindi kutoka meli kwenye Bahari Hindi Lilishindwa vibaya na Jeshi la Ulinzi wa Kijerumani chini ya uongozi wa Paul von Lettow-Vorbeck.

Mwaka 1922 "Tanganyika Territory African Civil Services Association" (TAA) iliundwa Tanga ambayo ilikuwa shirika ya kwanza ya Kiafrika yenye shabaha za kisiasa.

Kutokana na kupanuka kwa bandari ya Dar-es-salaam, umuhimu wa bandari ya Tanga umerudi nyuma.

3 comments:

Unknown said...

Nani kaandika hii historia? Seriously, tupeni jina lake.

Sisi wazaliwa na wenyeji wa mji wa Tanga tunajisikia kudhalilishwa kwa dhihaka hii iliyoletwa hapa kama historia ya mji wetu.

Ni bora mtu usiandike kitu kuliko kutudhihaki kiasi hiki.

Very much insulted.

Unknown said...

Moderators of this forum:

I am pleading with you to please remove this trash masquerading here as the history of Tanga city. Your blog is viewed worldwide and people may think this is an authentic history of Tanga.

If you can not remove it then at least give us the author's name and contact.

Unknown said...

Mwandishi wa hili bandiko amesema kuwa asili ya jina la Tanga ni lugha ya Kiajemi (Persian). Yafuatayo ni maneno ya Kiajemi yanayokaribia hili neno Tanga:

Tange = narrow straits (channel) mountain pass (Njia ya uchochoro milimani)
Tangna = ravine or gorge (korongo)
Tanha = alone (pekee)

Sasa ni neno gani hapa unalomaanisha ndio chanzo cha neno TANGA? Maneno yote haya hayana uhusiano wowote na muono wa bandari na kijiji cha Tanga wakati Waajemi walipokuja.

Unaweza kutupa citation ya unachokisema hapa.