ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 8, 2015

Mjumbe Hauwawi! Naiwakilisha jinsi ilivyo!

TAFAKARI EWE UNAYEJIITA MWANA CHADEMA 
----------------------------------------------
Inasikitisha sana kuona ukabila na undugu kama huu Tz...

1. Mwenyekiti Chadema taifa- Mh Freeman
Mbowe (mchaga,kilimanjaro)

2. Mkurugenzi wa fedha na uwekezaji - Ndugu
Anthony Komu (mchaga,kilimanjaro)

3. Mwenyekiti Bodi ya wadhamini ya chama -
Mh. Philemon Ndesamburo (mchaga,
kilimanjaro)

4. Mkurugenzi wa Rasilimali wa chama- Ndugu
Suzan Lymo (mchag,Kilimanjaro)

5. Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri -Ndugu
John Mrema (mchaga, kilimanjaro)

6. Naibu katibu Mkuu wa chama - John
Mnyika ( mpare wa kilimanjaro mwenye maskani yake Dar)

7. Mwenyekiti wa Wanawake Halima Mdee (Mpare wa Kilimanjaro mwenye maskani yake Dar es Salaam)

8. Makamu mwenyekiti wa Wazee Susan Lymo (mchaga wa Kilimanjaro)

9. Walinzi wote wa Mbowe (wachaga wa Kilimanjaro)

10. Asilimia 98 ya madereva wa Chama wachaga wa Kilimanjaro

Asilimia 80 ya wabunge wa kuteuliwa wa Chadema wanatoka Kilimanjaro na
Arusha,wakiongozwa na Mrs wa Mbowe wa pili Joyce Mukya, Grace Kihwelu, Suzan Lymo, Lucy Ndesamburo Owenya, Cecilia Pareso, Rebecca Mngodo na Rose Kamili.

11:Tundu Lisu MB na dada yake wa kuzaliwa MB
wa kuteuliwa,

12:Dk Wilbroad Slaa katibu mkewe wa ndoa Mb
wa kuteuliwa

13:Mbowe Mwenyekiti Mkewe mdogo Mb wa
Kuteuliwa

16:Ndesamburo Mb mwanawe wa kuzaa MB
kuteuliwa

16:Mtei Mlezi wa chama mkwewe Mbowe
Mwenyekiti wa Chama,
Hii familia inataka iongoze watu zaidi ya milioni
44 haitakuja kutokea katika historia ya Tanzania

Ndio wanafamilia hawahawa waliomtengenezea zengwe la kumfukuza Mh Zitto Kabwe katika chama hiki cha kifamilia baada ya kuona anakubalika ndani ya chama hicho na anauwezo wa kuwa mwenyekiti endapo angechuana na Mbowe lakini si mchaga wala mtu was kaskazini.

Hapo ndipo vikao vya kifamilia vikaanza na kuamua kumtimua Zitto.

Wanafamilia hawa ndio wamemuuzia chama chao Edward Lowassa kwa kiasi cha Billion 10 ili agombee urais kupitia chama hiki! Dr Slaa alipohoji akaambiwa wewe sio mwanafamilia hivyo tulikustili kwa muda tu. Ndipo slaa akagundua kuwa sio chama bali ni SACCOS na kuamua kujiengua.

Mwl Nyerere aliwahi kusema, nanukuu " Mtu anayeonekana anapenda sana kwenda ikulu hafai hata kidogo ni wa kukwepa kama Ukoma".

NDG watanzania huyu Lowassa anavyopenda sana kwenda ikulu tumkwepe. Hizo bilioni 10 alizonunulia chama anataka akazirudishe kwa kutuibia sisi wananchi. ZINDUKA!

Kama amenunua chama akipewa nchi siataiuza kurudisha gharama zake......!!!!?

‪#‎SayNo2Fisadi‬
‪#‎FisadiMwikoIkulu‬
‪#‎RestInPeaceFisadi‬
‪#‎NoEntryBigFisadi‬

JIUNGE NA KAMPENI HIZI KUIOKOA NCHI YETU

JOIN THE MOVE TO RESCUE OUR COUNTRY

21 comments:

Anonymous said...

Naona unataka kuleta mambo ya kikabila katika hii blog toa huu ujinga

Anonymous said...

Umeiandika ilivyo ndio mwisho wako umewadia huelewi uandishi na wala hujafanya mahesabu umekurupuka. CDM iko nchi nzima..umetumwaaah.

Anonymous said...

Inahusu nini hii
Mbona enzi Nyerere wengi walikuwa toka Mara au Musoma
Achani ubaguzi

James Bond said...

Kwa hiyo kuzinduka ni kuendeleza utawala wa CCM? Nasema hivi..hii blog ni hususan kwa wanadiaspora..sisi diaspora tuko huku kubadilisha kile kilichotuondoa nyumbani Utawala mmbovu wa CCM. .tunahitaji mabadiliko na hatujayapata ndani ya CCM kwa miaka 50..sasa kama wewe unasumbuliwa na sura ya Lowassa hilo ni tatizo lako lakini sisi tatizo letu ni CCM na tutaiondoa kwa hata kwa mkono wa Lowassa. .history iko wazi na mwenye macho haambiwi tazama. .CCM imezeeka tunahitaji mfumo mpya ambao utapatikana nnje ya CCM sio ndani ya CCM. .UKAWA ndiyo msiba wa CCM.

Anonymous said...

Hayo mambo yaliozungumzwa hapo juu yote ni ya ukweli kabisa. Chadema ni chama cha kikabila walichofanya ni kuchomekea baadhi ya mamluki ili kionekane chama cha kitaifa. Kile ni chama cha watu binafsi yaani mtei na familia yake wananchi wanazugwa tu.

Anonymous said...

Ndugu mwandikaji wa taharifa zinduka naomba tu tuache maneno ya uzushi.Tusianze kuingiza ukabila mahali haupo. Mh Edward Lowasa atakama ametoa billion 10 hiyo ni shukrani yake kwani tangu hapo Mh Lowassa yeye ni mchangiaji wa maendeleo ya wananchi. Ni kiongozi yupi Tanzania ameshaonyesha moyo wakuchangia maendeleo ya wananchi kama Mh Lowassa.Mimi naamini sana watu wenyeuwezo wakutafuta pesa kwani wanauwezo wakuona mbali.Naamini Mh Lowassa Akiwa rais Tanzania itakuwa na mwamko mpya na tutapiga atua. Ndugu Watanzania tujipe moyo. Tusiogope mabadiliko. Bila mabadiliko Tanzania hatutasonga mbele tutabakia pale pale. Tuangalie nchi kama Marekani vyama vinapokezana kila wakati, na ndio maana wanasonga mbele kwa mbele. Ni wakati wa CCM kuachia ngazi nao wakae bench na wao wakosoe. Wasikubali kukosolewa tu. Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote.

Anonymous said...

Ukabila ukiruhusiwa kuingia kwenye siasa Tanzania hakutakuwa na rais atakayetoka kwenye kabila dogo iwe ni CCM, CHADEMA au chama kingine.

Anonymous said...

UNAZUNGUMZA UPUUZI MTUPU. VIPI KUHUSU KIKWETE, SALMA NA RIDHIWANI MBONA WOTE WAJUMBE WA HALMASHAURI KUU YA TAIFA...SIYO HAYO TU NA HIZO NYUMBA NA BIASHARA ZA MATRILLIONI YA FEDHA WALIZOIBA KUPITIA EPA NA WIZI HUO UNAOENDELEA SERIKALINI? HII SERIKALI IMEIBA MATRILLIONI NA INAENDELEA KUIBA....KILA KITU NCHINI KINAANGAMIA KWA AJILI YA HUYU RAIS KIKWETE. MSIONGEE MSICHOKIFAHAMU. BAADA YA MUDA MTAONA MSOGA UTAKUWA KAMA GBADOLITE YA MOBUTU. UNAONGELEA NINI KUONA MTOTO WA KIKWETE ANAYEITWA SAID KUONEKANA KWENYE UJUMBE WA RAIS KIKWETE AKIWA NCHINI AUSTRALIA WAKATI HANA STATUS YA KIONGOZI WA SERIKALI?

Unknown said...

CCM imeanza kubaguana kwa misingi ya kikabilaBaada ya kushindwa kuwabagua kwa misingi ya kidini ambayo ilipelekea watu wengi kupoteza maisha hapa karibuni wakiwemo viongozi dini. Jeshi la wananchi wa Tz JWTZ 75% ni ndugu zetu wa Msoma; je, sisi siyo Wantanzania kwa sababu jeshi hilo linaongozwa na watu Msoma? Hiyo hoja ya ccm ni upungufu wa mawazo na kukosa sera. Hiyo ni hatari sana kuanza kubaguana hivyo, we are all one, awe mchaga, Mha, ndengereko kama anauwezo wa kuongoza sawa. Nyerere alikemia sana hilo na kama ccm wamekosa cha kuwambia Watanzania ni bora waondoke kimyakimya. Media muwe makini sana na habari mnazowafeed watu wakati huu, si kila habari lazima mzirushe. Mauaji ya kimbali ya Rwanda na Burudi mwaka 1994 yalichangiwa sana kwa 80% na media.

Anonymous said...

NAJUA HII HUTAITOA, KAMA ILIVYO KAWAIDA YAKO. UKWELI NI KWAMBA WATU WENYE MAWAZO HASI KAMA HUYU MTOA MADA HATA UKIWAPA NINI WATATAFUTA JINSI YA KUWEKA SHOMBWE.. KWA KIFUPI MTU YOYOTE ANAYETUMIA JICHO LA UKABILA AU UDINI KAMA HUYU MTOA MADA ANAWEZA KUONA MATATIZO KILA SEHEMU. MFANO UKIANGALIA CCM KAMATI KUU YOTE WAISLAMU, KASORO MAKAMU MWENYEKITI SASA NDIO TUSEMEJE? TUACHE TABIA ZA KUENDEKEZA UBAGUZI WA KIDINI, JINSIA, NA UBAGUZI WA AINA YOYOTE ILE, WATOA MADA KAMA HUYU NDIO WANAJENGA UBAGUZI, BADALA YA KUONA WATANZANIA YEYE ANACHAGUA UKABILA TUKEMEE TABIA HIZI HASI

Unknown said...

Baada ya kushindwa kuwabagua kwa misingi ya kidini ambayo ilipelekea watu wengi kupoteza maisha hapa karibuni wakiwemo viongozi dini. Jeshi la wananchi wa Tz JWTZ 75% ni ndugu zetu wa Msoma; je, sisi siyo Wantanzania kwa sababu jeshi hilo linaongozwa na watu Msoma? Hiyo hoja ya ccm ni upungufu wa mawazo na kukosa sera. Hiyo ni hatari sana kuanza kubaguana hivyo, we are all one, awe mchaga, Mha, ndengereko kama anauwezo wa kuongoza sawa. Nyerere alikemia sana hilo na kama ccm wamekosa cha kuwambia Watanzania ni bora waondoke kimyakimya. Media muwe makini sana na habari mnazowafeed watu wakati huu, si kila habari lazima mzirushe. Mauaji ya kimbali ya Rwanda na Burudi mwaka 1994 yalichangiwa sana kwa 80% na media.

Unknown said...

aliye andaa hii ni mpumbavu na haipendi nchi yake @team Lowassa 2015..

Anonymous said...

nafikiri ni chama na wengi ni wanajitolea,,pamoja na kupata ruzuku,,,kaazi ya kujenga chama inahitaji watu waaminifu,,,si suala la ukabila,,sababu akiongoza lowasa kuwa rais hana ukabila,,,na wala atashinikizwa na chadema,huo ni mtazamao wangu,,,

Anonymous said...

Asante mdau, umesahau kumtaja Financier wao Ndugu MENGI (naye ni MCHAGA). Ametumia mamilioni kuijenga Chadema. Unfortunately, hawataweza kuinunua nchi yenye makabila 120. Wanaweza kuwanunua Wachaga, Wapare, Waarusha, Wamasai, Wameru, na baadhi ya Wahaya(Ndumakuwili wachache), lakini hawatayanunua makabila mengine (majority). Pia, ukweli ni kwamba hao Wachaga wamejijenga kwa nguvu kwenye mitandao ili kuipigia Chadema debe, hilo limejulikana toka siku nyingi. Sidhani Rais wa Tanzania atatokea Mikoa ya kaskazini anytime soon, kwa sababu wananchi wachache nchini wanawaamini (have no faith) na watu wa kaskazini (esp.Chagas and pares) kutokana na Nepotism ambaye imekuwepo toka tupate Uhuru. Naweza kuandika kitabu kutafakari kauli hii. Hivyo, uliyoyaandika mdau hapo juu, is just a summary ya Chadema, details nyingi Watanzania wanazijua kuhusu CHADEMA na UKABILA (exclusive Northern zone club)!.

Anonymous said...

Ulichoandika kinadhihirisha jinsi ulivyo na uelewa mdogo wa mambo. Na uongo unaouweka huku ni kujifurahisha tu hakuna ukweli wowote. Endelea kutetea chama cha majambazi waliokwishafika ICU na madaktari Wako kwenye Mgomo!!

Anonymous said...

Nawasifu sana Watanzania kwa kuwa mahili na wenye uwezo mkubwa wa kuelewa mambo yanayoisibu nchi yetu. Ukweli ni kuwa mengi yatasemwa na kati ya hayo yako yatakubalika na mengine kukanushwa lakini yote haya Watanzania wanayafahamu. Kama wahenga walivyonena "vitendo vinaongea zaidi kuliko maneno" au kwa lugha ya wenzetu "actions speak louder than words" hivyo Watanzania katika maamuzi yao watazingatia zaidi vitendo ambavyo wanaviona na wala sio ushabiki wa maneno mnayoyandika humu kwenye mtandao. Na kwa sisi tulioko huku ughaibuni haitatusaii sana kuwaelemisha Watanzania walioko nyumbani kwani haya yote tunayoyaandika kutoka huku ughaibuni hatuyaelewi zaidi kuliko ndugu zetu walioko huko nyumbani. Mwisho, sio kweli kuwa wote tulioko huku ughaibuni tuko huku kubadilisha kile kilichotuondoa nyumbani Utawala mmbovu wa CCM. Wengi wetu tuko huku kwa sababu mbalimbali kama, vile; kimasomo, kiajira na maslahi na vinginevyo.

Unknown said...

Sasa jamani mtoa mada alisha sema mjumbe hauwawi kwanini tena mnataka kumpa kibano. Mtoa mada ni mzalendo wa kweli tu kama tulivyo watanzania wengi siku zote tupo macho kuhakikisha kwamba siku zote tutaongozwa na utanzania wa mtu na uwezo wake wa kuongoza sio ukabila. Binafsi naipa pongezi CCM kwa kuwa chama kinachowakilisha watanzania kwa asilimia mia moja 100%. Hakuna kona ya Tanzania usipoikuta CCM tena katika watanzania wa aina tofauti. CCM haiwezi kuondoka madarakani kwa kusema tu chama cha majambazi huko ni kuishiwa hoja. Kama CCM ni chama cha majambazi Lowasa ni miongoni mwa majambazi wakubwa kwa sababu karibu maisha yake yote kayatumikia CCM sasa leo ni kiongozi wa chadema. Sasa itakuwa kaacha ujambazi kafuata ukabila? Nafikiri watanzania tunao uwezo wa kuuzibiti ujambazi ukabila itakua shida tutaikata nchi vipande vipande. Lakini to be honest hasa kwa sisi tunaoishi huku nje nazungumzia hasa tunaoishi hapa marekani naamini upeo wetu wa kuona mambo hasa ya siasa ni mpana zaidi tunaona magavana na viongozi wa uma wanapojizulu kwa tuhuma za ngono tu. Sasa mtu kama LOWASA ana kashfa zilizomzunguka za ubadhirifu wa kutisha wa mali ya uma halafu ati anagombea uraisi sisi waafrika ni watu aina gani? Kweli tunataka mabadiliko lakini sio kila mabadiliko ni ya maana. Kwangu mimi magufuli ni mtu sahihi zaidi ya Lowasa bila ya kujali anatoka wapi na ni kiongozi ambae ataleta mabadiliko ya kweli Tanzania. Si mtizami magufuli kama anatoka CCM au CHADEMA namtazama magufuli kama muwajibikaji mzuri na ni mtu ambae kila siku anafikiria kutimiza majukumu yake. Na si mtu wa sisa zaidi kama lowasa kwa maana ya kwamba magufuli amekuwa mtendaji zaidi kwenye serikali kuliko kwenye chama.

Unknown said...

Umbeya huu hatuutaki,kwani watanzania wamechoka kufa maskini ndani ya CCM,tunataka mabadiliko..tena msanifu huyu aondoe huo uchafu wako hapo juu kama na wewe umenunuliwa sema??wasomi wengi wanaona mbali wako upinzani?/wewe ulie tu?Lowassa lazima awe Rais nasafirisha 20Million dollars kuwasaidia wapinzani kuondoa hilo sugu CCM/lenye mfumo wa ufisadi,kulindana maslahi na kuchota cha maskini tax zao sasa basi ama la na utaendelea kuwa maskini kama sera yako hapo juu hutaipiga mawe ife.

Anonymous said...

NI KWELI WATANZANIA WATAAMUA, KWA KUZINGATIA UBOVU WA BARABARA, HUDUMA MBOVU ZA MAHOSPITALIN, USAFIRI USIO UHAKIKA, RUSHWA, MIGOGORO YA ARDHI, MATUMIZI MABOVU YA MADARAKA NA MAMBO KADHA WA KADHA YANAYOFANYWA CHINI YA UTAWALA WA CCM. PIA NI KWELI SISI TUPO HUKU KWA SABABU MBALIMBALI KAMA VILE KUFUATA ELIMU BORA KULIKO ELIMU MBOVU IAYOSIMAMIWA NA CCM, KUTAFUTA AJIRA, SABABU CCM IMESHINDWA KUSIMAMIA MISINGI BORA YA UCHUMI UNAOTOA AJIRA KWA WATU WAKE, MASLAHI KWA SABABU NYUMBANI KUMEHARIBIWA NA CCM KWA HIYO HAKUKALIKI ...MTO HOJA HAPO JUU NAKUUNGA MKONO...TEH TEH TEH

Anonymous said...

Kinachonishangaza ni uwezo mkubwa wa watanzania katika kujitoa fahamu. Kuwa CCM au Chadema haina maana ndio ushabiki kila kitu.
Mada iliyoletwa ni valid na ni ya kweli . nepotism,ufisadi upo CCM na Chadema vilex2. Huu ni ukweli. Tafuteni hoja zingine za kubishana, I believe hata leo hii Chadema ikichukua nchi haitaweza kupambana na ufisadi na nepotism mambo yatakuwa ni yalex2

Anonymous said...

WEWE MTOA MADA WA MWISHO SASA UNATAKAJE? WATU WANYAMAZE ILI MAMBO YABADILIKE? AU BADO UNAIMANI NCHI IENDELEA KUTUMIA WATU WALE WALE MBINU ZILE ZILE . JAMANI TUJARIBU KUANGALIA HOJA ZETU NA TUACHE UOGA WA MABADILIKO . HIZI KAULI ZA KUSEMA KUWA CHADEMA WATAFANYA KILE KILE NI KAULI ZA UOGA NA ZAKUOGOPA MABADILIKO. KWA KIFUPI MABADILIKO NI MUHIMU NA WAKATI NI SASA, WEWE ENDELEA KUJIFICHA UKINGOJEA HOJA ZA KIBIASHARA.