Advertisements

Monday, August 3, 2015

NGOMA AFRICA BAND WAFANYA KWELI MJINI LIGA,NCHINI LATVIA


Liga,Latvia
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band maarufu kama
FFU ughaibuni ukipenda waite viumbe wa ajabu Anunnaki Alien juzi wikiendi walifanikiwa kuwadatisha washabiki wa muziki nchini Latvia katika maonyesho ya Summer Festival,yaliyofanyika Liga. bendi maarufu yenye makao yake nchini Ujerumani inayoongozwa na mwanamuziki mahili Ebrahim Makunja aka Kamanda Ras Makunja,imejizolea umaarufu wa kimataifa kwa kutumia mdundo wake wa "Bongo Dansi" uliochanganywa na rumba la kukata na shoka mdundo huo umefanikiwa kuwazoa na kuwadatisha akili washabiki wengi wa kimataifa.
Ngoma Africa Band kwa sasa wanatamba na single CD yao mpya 'La Mgambo"
yenye mbili za kumuaga rais JK.



No comments: