Advertisements

Monday, August 3, 2015

RUNGWE ACHUKUA FOMU YA KUGOMBEA URAIS LEO JIJINI DAR ES SALAAM

Mgombea Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe akipokea fomu ya kugombea urais kutoka kwa Afisa Mwandamizi Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Adam Nyando katika ofisi za NEC leo jijini Dar es Salaam.
Mgombea Urais wa Chama Cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kuchukua fomu za kugombea Urais kwa tiketi ya CHAUMA nje ya ofisi NEC leo jijini Dar es Salaam. (Pichana Emmanuel Massaka)
Na Chalila Kibuda
 MWENYEKITI wa Chama cha Ukombozi na Maendeleo (CHAUMA), Hashim Rungwe amechukua fomu ya kugombea urais katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.

Akizungumza baada ya kuchukua fomu hizo Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), leo jijini Dar es Salaam, Rungwe amesema watanzania kama wanahitaji maendeleo wachague chama hicho na sio kuchagua watu wanaotaka kutumikia matumbo yao. Amesema zoezi la kuchukua fomu za urais ziko wazi na kutufanya wagombea kuwa huru katika zoezi zima kutoka na maandalizi yalifanywa na tume ys Taifs ys Uchaguzi.

Rungwe amesema mwaka 2015 aligombea kwa tiketi ya Chama cha NCCR-Mageuzi lakini kura hazikutosha na kufanikiwa kupata wabunge wawili kwa tiketi kwa chama hicho. Amesema ana uwezo wa kuwatumikia watanzania na sio kwenda Ikulu kwa ajili ya kutafuta jinsi ya kujinufaisha na kuwaacha watu walionipa ridhaa ya kuwaletea maendeleo.

Aidha amesema nafasi ya urais sio ya mchezo kutoka na na kuwa majukumu makubwa ya kuwatumikia watu katika kuwapa maendeleo yatayotokana nafasi hiyo.

 “Nina imani watanzania wataichaugua CHAUMA katika kuperusha bendera katika kuweza kupata maendeleo kama kauli mbiu ya chama kutaka ukombozi” anasema Rungwe. Vyama vilivyochukua fomu ya urais vimefikia vinnea mbavyo ni, Chama cha Tanzania Labour Party (TLP), UPDP, Chama cha Democratic Party (DP), pamoja na Chauma.

Mgombea wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Pombe Magufuli anatarajia kuchukua fomu kesho katika Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), jijini Dar es Salaam. mwisho


No comments: