Advertisements

Tuesday, October 6, 2015

KARATE SEMINA, LEEDS, ENGLAND.

 Mwakilishi wa Jundokan So Honbu Tanzania, sensei Fundi, 3rd Dan, amearikwa kushiriki moja ya semina ( Gasshuku) ya Karate mtindo wa Okinawa Goju Ryu Karate-Do Jundokan So Honbu. Semina hii itafanyika nji wa Leeds, Uingereza, kuanzia tarehe 16 hadi 18 Oktoba, 2015. Wakuu wa Jundokan toka visiwa vya Okinawa wakiwemo; Sensei Yoshihiro Miyazato, Kancho ambae ni mtoto wa mwanzilishi wa Jundokan dojo mwaka 1957 master Eiichi Miyazato ( aliyekuwa mwalimu wa Sensei Bomani toka mwaka 1968), ndie mwenyekiti wa sasa wa Jundokan So Honbu Dojo ataongoza wajumbe toka Okinawa; Sensei Tsuneo Kinjo 9 Dan, Gima Sensei 9 Dan, Sensei Yurio Nakada 9 Dan na masensei wakuu wa Jundokan matawi ya Ulaya yote. Sensei Fundi, atakuwa mtanzania pekee kuwakilisha tawi la Tanzania. Pia, Sensei Fundi, alipata fursa ya kuwa na wakuu hao mwezi wa juni mwaka huu alipotembelea visiwani Okinawa, katika mji wa Naha. Mbinu za Karate, Kata Bunkai ( Tafsiri za kutumia mbinu za mapambano za kujilinda) na maendeleo yake duniani ni moja ya mambo yatakayo jadiliwa katika semina hiyo

No comments: