Saturday, October 24, 2015

PONGEZI KWA CHAMA CHANGU

Loveness Mamuya, mratibu wa CCM Marekani

Baada ya kuangalia na kufuatilia mikutano ya kampeni kama kada wa chama cha mapinduzi anachukua nafasi hii kukipongeza Chama chake Chama Cha Mapinduzi kwa kuendesha kampeni zilizofuata misingi ya demokrasia, pia nawapongeza mh Dr John P. Magufuri na mama Samia Suluhu kwa kuweza kuzunguka Tanzania nzima kuwafikia watanzania wote kila kona, Ali Shein pia kwa upande wa Zanzibar. Nachukua nafasi hii kuwakumbusha watanzania wenzangu kujitokeza kuwapigia kura Rais mh John P. Magufuli na makamu wake mama Samia Suluhu, Ali Mohamed Shein, wabunge na madiwani wa CCM kwani ni hakika wanatosha hasa kwa kiongozi wetu Magufuli tutapata wabunge waadilifu, watendaji na wazalendo. Tutumie haki yetu ya demokrasia tupige kura na tuwasaidie wale yale makundi yanayohitaji msaada. Mungu ibariki CCM, Mungu ibariki Tanzania.