ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 22, 2015

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI MAZISHI YA DADA YAKE RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE KIJIJINI MSOGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akipokelewana Mke wa Rais Mstaafu Mama Salma Kikwete,wakati alipowasili kwenye msiba wa Dada yake na Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete, jana kijini Msoga Mkoa wa Pwani. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiwafariji baadhi ya wanafamilia wa Marehemu Tausi Khalfani Kikwete, aliyekuwa Dada yake na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, kijijini Msoga wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani jana Desemba 21, 2015
Makamu wa Rais Mstaafu,Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, wakati alipowasili Kijiji cha Msoga Wilaya ya Chalinze, jana Desemba 21, 2015 kwa ajili ya kumfariji kwa kufiwa na Dada yake Bi Tausi Khalfan Kikwete
  Rais Mstaafu Dkt.Jakaya Kikwete (kulia) Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, wakizungumza wakati wakiwa kwenye shughuli za msiba wa Dada yake na Dkt. Jakaya Kikwete, Bi Tausi Khalfan Kikwete, Kijiji cha Msoga Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani, jana Desemba 21, 2015
Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akisalimiana na Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete, wakati alipowasili Kijiji cha Msoga Wilaya ya Chalinze, jana Desemba 21, 2015 kwa ajili ya kumfariji kwa kufiwa na Dada yake Bi Tausi Khalfan Kikwete
Rais Dkt.John Pombe Magufuli (wa pili kulua) akizungumza na Rais Mstaafu Dkt Jakaya Kikwete (kulia) wakati wakiwa kwenye shughuli za msiba wa Dada yake na Dkt. Jakaya Kikwete, Bi Tausi Khalfan Kikwete, Kijiji cha Msoga Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani, jana Desemba 21, 2015. Kushoto ni Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (wa pili kushoto) na Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, (wa pili kushoto) Mke wa Rais, Mama Janeth Magufuli, wakijumuika na baadhi ya waombolezaji kwenye msiba wa aliyekuwa dada yake na Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, marehemu Tausi Khalfan Kikwete, aliyezikwa jana Desemba 21, 2015 Kijiji cha Msoga Wilaya ya Chalinze Mkoa wa Pwani
Baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu, wakimswalia marehemu Tausi Khalfan Kikwete, jana Desemba 21, 2015, Kijiji cha Msoga Wilaya ya Chaline Mkoa wa Pwani
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Luhaga Mpina,akishiriki kubebe jeneza lenye mwili wa marehemu Tausi Khalfan Kikwete wakati wakielekea makaburini kwa mazikojana Desemba 21, 2015.

No comments: