
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mheshimiwa January Makamba (wa kwanza kulia), akisikiliza jambo kutoka kwa Mgeni wake, Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini, Bi Bella Bird (katikati), wakati alipomtembelea Waziri huyo ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa kwake Uwaziri. Wa kwanza kushoto katika picha ni Bwana, Andre Bald aliyeongozana na Mkurugenzi huyo .

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Mheshimiwa, January Makamba (katikati), akizungumza wakati alipotembelewa na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini, Bi Bella Bird kwa ajili ya kumpongeza kwa kuteuliwa kwake Uwaziri. Wa kwanza kushoto katika picha ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Dkt. Julius Ningu akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo Bwana Sazi Salula, huku wa kwanza kulia ni Bwana Andre Bald aliyeongozana na Mkurugenzi wa Benki ya Dunia Nchini.
(Picha na OMR)
No comments:
Post a Comment