ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 22, 2015

Waziri Mahiga apokea Nakala ya Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Korea


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Jamhuri ya Korea nchini, Mhe. Song Geum-young. Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 21 Desemba, 2015.

Mhe. Dkt. Mahiga akiwa kwenye mazungumzo na Balozi Song Geum-young mara baada ya kupokea nakala za hati za utambulisho.

Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (kushoto) akiwa na Bw. Thobias Makoba (kulia), Msaidizi wa Waziri pamoja na Bw. Khatib Makenga (katikati), Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo kati ya Dkt. Mahiga na Balozi Song Geum-young (hawapo pichani)

Kaimu Mkuu wa Itifaki katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Bw. James Bwana akimpatia utaratibu Balozi Song Geum-young kabla ya kuwasilisha Nakala zake za Utambulisho kwa Mhe. Waziri

No comments: