ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, December 22, 2015

Waziri Mahiga apokea Nakala ya Hati ya Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa EU


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga akimkaribisha Balozi Mteule wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini, Mhe. Roeland Van De Geer alipofika Wizarani kwa ajili ya kuwasilisha Nakala za Hati za Utambulisho kwa Mhe. Waziri. Tukio hilo lilifanyika Wizarani tarehe 21 Desemba, 2015.

Mhe. Dkt. Mahiga akipokea Nakala za Hati za Utambulisho kutoka kwa Balozi Mteule wa Umoja wa Ulaya hapa nchini, Mhe. Roeland Van De Geer.

Mhe. Dkt. Mahiga akizungumza na Balozi Mteule wa EU, Mhe. Roeland Van De Geer

Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirkiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Joseph Sokoine akiwa na Bi. Felister Rugambwa wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Dkt. Mahiga na Balozi Roeland Van De Geer (hawapo pichani) 



No comments: