ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, January 28, 2016

TANZANIA YATOA WITO WA KUACHIWA FURSA YA KUPANGA NA KUCHAGUA MIRADI YA MAENDELEO

Balozi Tuvako Manongi , Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza wakati wa mkutano wa Bodi ya Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu ( UNFPA) uliofanyika siku ya jumatano ukiwa ni mwendelezo wa mikutano ya Bodi za UNDP. UNOPS, na UNICEF. Katika mchango wake Balozi ametoa wito kwa washirika wa maendeleo kuwapa nafasi watendaji wa serikali kupanga na kuchagua miradi ya maendeleo. Pamoja naye ni Maafisa wa Uwakilishi, Bw. Songaliel Shilla, Bi. Lilian Mukasa na Bi. Ellen Maduhu.
Meza Kuu akiwamo Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA Dr. Babatunde Osotimehin wakimsikiliza Balozi Tuvako Manoni, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa wakati ambapo pamoja na mambo mengine amesisitiza dhana ya uwajibikaji wa pamoja kati ya serikali na washirika wa maendeleo
Dr. Babatunde Osotimehin, Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA akiwasilisha taarifa yake mbele ya wajumbe wa Bodi ya UNFP, anaonekana Balozi Tuvako Manongi akifuatilia kwa karibu taarifa ya mtendaji huyo aliyoitoa mwanzoni mwa mkutano kabla ya wajumbe wengine kupewa fursa ya kuchangia.
Sehemu wa Wajumbe wa mkutano wa Bodi ya UNFPA, mkutano ambao pia umepitisha Taarifa za Baadhi ya Nchi ( Country Report)Tanzania ikiwamo


Na Mwandishi Maalum, New York

Tanzania imetoa wito kwa washirika wa maendeleo yakiwamo Mashirika ya Umoja wa Mataifa kuiachia nafasi ya kupanga na kuchagua miradi yake ya maendeleo kwa kuzingatia vipaumbele vyake.

Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi, katika siku ya pili ya Mkutano wa Bodi za Mifuko na Mashirika ya Umoja wa Mataifa ambapo katika siku hiyo ya Jumatano Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Idadi ya Watu ( UNFPA) uliwasilisha Taarifa yake iliyobainisha mafanikio pamoja na changamoto za utekelezai mipango yake ya maendeleo.

Balozi Manongi, amewaeleza wajumbe wa Bodi hiyo, ambayo Tanzania pia ni miongoni wa wajumbe kwamba, Tanzania inaamini kuwa ushirikiano wa kweli ni ule ambao washirika watazipatia mamlaka za serikali fursa ya kupanga na kung’amua vipa umbele vyake vya maendeleo.

Katika mkutano huu pia iliwasilishwa Taarifa ya nane ya Tanzania ( country progamu) ambayo inaainishia miradi itakayotekelezwa na UNFPA kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia 2016 hadi 2021.

Pamoja na kusisitiza haja na umuhimu wa mamlaka za kitaifa kuachiwa fursa ya kupanga na kuamua miradi ya maendeleo, Mwakilishi huyo wa Tanzania pia amebainisha katika mchango wake kwamba suala la uwajibikaji nalo linapashwa kuwa kwa pande zote.

Vile vile amesema , Tanzania ingependa kusisitiza juu ya hoja ya uwazi, uwajibikaji katika ufadhili na uthibitisho wa thamani ( value for money) ya miradi inayofadhiliwa na Mfuko huo.

Balozi Manongi amebainisha pia kwamba, tatizo la uendelevu wa miradi inayoazishwa na washirika wa maendeleo ni moja ya changamoto inayozikabili nchi nyingi. Na kuongeza kuwa changamoto hiyo inakwenda mbali zaidi ya miradi inayofadhiliwa na UNFPA.

“Itakuwa jambo jema na la muhimu kama mafanikio tunayoyapata kutokana na utekelezaji wa miradi ya maendeleo si tu yanakuwa endelevu lakini pia panakuwepo na ushahidi wa mafanikio yake.”akasema Balozi

Kuhusu uwezeshwaji wa taasisi mbalimbali za kitaifa ikiwano zile zinazohusu ukusanyaji na uchambuzi wa takwimu, Tanzania imesema haitoshi kwa Mashirika ya Kimataifa kutoa tu kasoro au mapungufu katika eneo hilo bila ya kuainisha namna gani ya kusaidia kutatua kasoro hizo.

Na kwa sababu hiyo Tanzania kwa kutambua umuhimu wa takwimu katika upangaji wa miradi ya maendeleo na mipango mingine, ingepeza kuona panakuwwepo na ushirikiano wenye tija na wadhati katika eneo la la uwezeshaji wa taasisi za kitaifa.

Akaongeza kwamba Serikali ya Tanzania inashukuru pale ambapo baadhi ya wadau wa maendeleo wamekuwa wakisaidia katika eneo hili. Na kwamba mafanikio mengi ambayo hata washirika wa maendeleo wanajivunia yamewezekana kutoka na serikali kutoa ushirikiano wake.

Akizungumzia kuhusu uhusiano na ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na UNFPA, Balozi Manongi pamoja na kueleza kwamba tofauti na huko nyuma hivi sasa uhusiano huo sasa umeimarika licha ya kupitia changamoto nyingi.

Akabainisha kuwa mazingira mazuri ya ushirikiano kati ya pande hizo mbili yamesaidia katika utekelezaji na ufanikishaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwano inayohusua masuala ya afya ya uzazi salama na uzazi wa mpango, udhibiti wa magonjwa kama vile ukimwi, na utoaji elimu mbalimbali kwa vijana iliwaweze kujitambua.


No comments: