Waziri Mkuu, Kassim Mjaliwa
akimkabidhi Balozi wa Namibia nchini aliyemaliza muda wake, Mhe. Japhet
Isaack zawadi ya ramani ya Tanzania iliyochongwa kwenye mti wa
mpingo ili aendelee kuikumbuka Tanzania atakapoondoka. alozi
alikwendaofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam, Januari 8, 2016
kuaga.
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amekuaana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Namibia ambaye anamaliza muda wake, Bwana Japhet Isaack.
Akizungumza na Balozi Isaack leo ,ofisini kwake ,Magogoni jijini Dar es salaa, Waziri Mkuu ameshukuru Balozi huyo na kumumwomba waendeleze uhusiano mwema ulipo baina ya nchi hizi mbili ambao ulianza tangu enzi za kugombania uhuru ili kusaidia kukuza uchumi wa nchi hizi mbili.
“Namibia ni nchi yenye uchumi uanaokua haraka, na mmefanikia katika baadhi ya sekta , hivyo ningependa Tanzania ijufunze kutoka kwenu hasa katika sekta za Utalii, Afya, na Elimu,” alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Pia, alitumia fursa hiyo kuwakaribisha raia wa Namibia kuja kuwekeza nchini katika maeneo mbalimbali ikiwemo viwanda na kuendeleza maeneo ya ukanda maalum ya uwekezaji (EPZ) ili kuongeza thamani ya mazao pamoja na kutatua tatizo la ajira nchini.
Kwa upande wake, Balozi Isaack amesema kwa kipindi alichokaa Tanzania amejifunza mengi, na amefurahishwa ambavyo Waziri Mkuu pamoja Serikali kwa ujumla inavyofanyakazi kwa kasi na kwa mafanikio makubwa.
“Hongera, ninafurahishwa na unavyofanya kazi hongera sana”, alisema Balozi Isack. Pia, amefurahi sana kipindi chote alichokaa Tanzania kwani kimekuwa na matukio mengi yenye kumbukumbu nzuri kwake.
Balozi Isack ameomba mahusiano ya nchi hizi mbili yaendelezwe ili zishirikiane zaidi katika masuala mbalimbali ya kukuza uchumi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
S. L. P 3021,
11410 DAR ES SALAAM
IJUMAA, JANUARI 8, 2016.
No comments:
Post a Comment