Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
MAKONDA ADAI HATA AKIFA AMESHAFANIKIWA, ATANGAZA VITA KALI NA WAUZA UNGA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ametangaza vita kali kwa watu wanaojihusisha na dawa za kulevya mkoani humo.
Akiongea leo jijini Dar es Salaam na viongozi wa serikali wa ngazi mbalimbali wa Mkoa huo, Makonda aliwataka viongozi wa ngazi za chini hususan Wenyeviti wa Mitaa kushirikiana kwa karibu na Jeshi la Polisi kuwabaini watu wanaojishughulisha na dawa za kulevya.
Mkuu huyo wa Mkoa ameweka wazi kuwa hivi sasa haogopi kufa kwa kuwa tayari alimeshayafikia mafanikio aliyoyahitaji hivyo ni bora afe akipigania Taifa lake. Amewataka viongozi wenzake pia kutoogopa kufa kwakuwa lazima watakufa bali kinachoangaliwa ni sababu za kifo.
Amewataka wenyeviti wa mtaa ambao ndio wanaishi kwa karibu zaidi na wananchi waweze kuwasiliana moja kwa moja na wakuu wa wilaya pamoja na wakuu wa polisi kwa njia ya simu za mkononi ili kuwajulisha kuhusu vitendo vya kihalifu vinavyoendelea katika maeneo yao.
Katika kuhakikisha Jeshi la polisi linapata ari zaidi ya kufanya kazi ya kudhibiti uhalifu, Makonda amesisitiza kuwa atakuwa anatoa motisha ya shilingi milioni moja kwa polisi atakayeonekana kufanya vizuri zaidi.
“Polisi atakayefanya vizuri… mimi nitawapa shilingi milioni moja kila baada ya miezi mitatu kwa kuwashindanisha,” amesema Makonda.
2 comments:
Sina uhakika na hili lakini wakati umefika wa kuwakamata na kuwachuchukulia hatua za kisheria tena kali hata wale wateja wanaotumia hayo madawa ya kulevya ili imfanye mtu anaeamua kuwa teja afikirie sana kabla ya kujiingiza katika upuuzi huo. Kwa nini sheria iwe kwa wale wauzaji wa madawa tu na kuwaacha wale wanaowashawishi kufanya hiyo biashara madawa wakisinzia mitaani tena wakati wa kazi? Nadhani katika kutangaza vita ya kweli basi mpaka mateja nao wakamatwe wapimwe na ikithibitika anatumia madawa ya kulevya afunguliwe mashitaka na si kufunguliwa mashitaka tu bali wao wawe ni moja ya chanzo cha uhakika cha kujua hayo madawa yanatoka kwa nani na isijali hilo teja ni mtu wa aina gani,awe super star hao ndio wawe wa kwanza kukamatwa kwa kuwa wao huwa na mvuto mkubwa katika jamii hasa vijana ambao wanawachukulia wao kama watu wa mfano katika maisha yao ya kila siku. Awe mtoto wa mkubwa au kigogo serikalini kamata tu sheria ni msumeno nadhani muheshimiwa Makonda ni kijana na utakuwa na weledi zaidi nnachokizungumza kwani wakati wa kulea maradhi umekwisha ni wakati wa kutibu sasa na kunako kutibu kama itatokezea mguu kukatwa ili kuzuia maradhi kutoenea mwili mzima basi hapana budi inabidi mguu ukatwe. Siku zote dawa haiwi kitu kitamu. Hata vyakula vingi vyenye siha zaidi kwa binaadamu ni vile vyakula vyenye ladha tata.kwa hivyo watanzania hatuna budi kuunga jitihada za muheshimiwa Makonda.
asante mkuu, ila wakati haya madawa yanauzwa kwa wingi bado serikali iliyokuweka madarakani baada ya kuutafuta kwa kujinadi sana yalikuwa yanaendelea ilikuwa bora sana ungemueleza akaweka mkazo lakini nadhani ulikuw aunaogopa kwani ilikuwa sio serikali ya ukweli na uwazi.
Nirudie tena kusema asante na kwa maana umeona mkubwa wako wa kazi JPM msisitizo wa kazi na kuwajibikabila kuona aibu basi nadhani unaelewa maeneo yale muhimu hasa magomeni, masaki wilaya uliyoongoza ikiongoza kwa hayo madawa na wenye mtandao ni waliokuw wakubwa na hadi leo wakubwa zako hivyo jitahidi mdogo wangu labda utaweza kufanikiwa kwani wajanja nii wengi, ila usifanye pupa kwnai nao wanajua sana !!
Post a Comment