ANGALIA LIVE NEWS

Friday, March 25, 2016

MBIVU MBICHI MGOGORO WANANCHI, ACACIA APRILI 5

Hatima ya mgogoro kati ya wananchi na mgodi wa Acacia North Mara katika eneo la Nyamongo wilayani hapa Mkoa wa Mara itajulikana mwezi ujao baada ya kamati ya uchunguzi iliyoundwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kukamilisha kazi yake. Kamati hiyo iliyoundwa mwezi mmoja uliopita, leo ilikabidhi ripoti ya uchunguzi wake kwa Waziri Muhongo.
“Aprili 11, ndiyo siku wizara itatoa uamuzi kuhusu njia ya kutatua mgogoro kati mgodi wa Acacia North Mara na wananchi hao wanaoishi kuzunguka eneo hilo,” amesema Profesa Muhongo baada ya kupokea ripoti hiyo.
Amesema Serikali itatekeleza mapendekezo ya kamati hiyo kufikia suluhisho la kudumu la msuguano kati ya wananchi na mwekezaji wa mgodi huo.
“Upande ambao hautaridhika na uamuzi wa wizara itabidi utumie mkondo na vyombo vingine kutafuta haki yao.
Mwenyekiti wa kamati wa hiyo, John Mayopa alisema kamati yake ilikuwa na wajumbe 27 waliotoka makundi mbalimbali ikijumuisha wataalam, viongozi na wananchi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mgodi.
“Kamati ilipitia nyaraka mbalimbali na kuwahoji wananchi 4,400 kutoka kata za Kibasuka, Matongo, Kemambo, Nyamwaga na Muriba zinazozunguka mgodi,” amesema Mayopa.
Februari 10, mwaka huu, Profesa Muhongo aliunda kamati kuchunguza na kubaini ukweli wa kero za wananchi dhidi ya mgodi huo.

No comments: