Naibu Waziri wa Sayansi na Tekinologia, Injinia Ester Manyanya akihutubia.Manyanya akiendelea kuhutubia wanafunzi, na wadau kuhusu tatizo la usonji.… akimsaidia kumsukuma mtoto mwenye usonji.
Maandamano ya maadhimisho hayo.
Naibu Waziri wa Sayansi na Tekinologia, Injinia Ester Manyanya leo amehudhuria maadhimisho ya Siku ya Watu wenye Usonji ambayo hufanyika Aprili, 2 kila mwaka nchini.
Maadhimisho hayo yamefanyika katika Viwanja vya Shule ya Al Muntazari, Ukonga jijini Dar yakihudhuriwa na wadau mbalimbali.
Hata hivyo mgeni rasmi, Waziri Manyanya alisema pamoja na gharama kubwa ya kuwasomesha watoto wenye tatizo la usonji lakini serikali imejipanga kupambana na watu wanaowanyanya sawa watu wenye usonji pamoja na kuwanyanyasa.
“Usonji ni ugonjwa kama magonjwa mengine na si laana kama watu wanavyodhani, serikali itapambana vikali na watu wanaowanyanyapaa pia wana haki ya kupata elimu kulingana na mahitaji yao kama watu wengi,” alisema waziri Manyanya ambaye alimuwakilisha Makamu wa Rais, Samia Suluhu.
Manyanya akihojiwa na wanahabari (hawapo pichani).
Kikundi cha Skauti ya watoto wa Shule ya Al Muntazari, Ukonga jijini Dar.
NA GABRIEL NG’OSHA/GPL
No comments:
Post a Comment