Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (aliyevaa koti) akishangiliwa na mamia ya wananchi wa Kata ya Sumbugu wilayani Misungwi mara baada ya kuwasili katika eneo hilo kwa ajili ya kufungua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi hao. Waziri Kitwanga ameanza ziara jimboni humo leo. Picha zote na Felix Mwagara.
Meneja wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mamlaka ya Maji Kahama na Shinyanga (Kashwasa), Denis Mlingwa akimuonyesha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi, Charles Kitwanga (kushoto) sehemu ya kuchukulia dawa ya Kituo kipya cha Afya cha Ihelele jimboni humo kinachotarajiwa kufunguliwa hivi karibuni kiweze kutoa huduma kwa wananchi wa eneo hilo. Kituo hicho kitaongozwa na Kashwasa wakishirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (aliyevaa koti) akicheza ngoma ya Kisukuma iitwayo Wachwechi wakati alipofanya ziara katika Kijiji cha Lutalutale, Kata ya Mbarika jimboni humo
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga akizungumza na wananchi wa Kata ya Mbarika jimboni humo wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuzungumza na wananchi katika kata hiyo.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Misungwi mkoani Mwanza, Charles Kitwanga (kushoto) akimkabidhi mpira wa miguu Mwakilishi wa Kitongoji cha Kashishi, Kata ya Sumbugu, Lucas Chai. Mbunge huyo alitoa mipira ya miguu katika kata mbalimbali jimboni mwake
No comments:
Post a Comment