ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, June 18, 2016

MAALIM SEIF KUONGEA NA WATANZANIA DMV

Mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Katibu Mkuu wa Chamba Cha Wananchi (CUF)  na Makamo wa Kwanza Mstaafu wa Rais wa Zanzibar, Simba wa Nyika - Maalim Seif Sharif Hamad, atanguruma hadharani ambapo pamoja na mambo mengine, ataelezea kwa kina na kama kawaida yake kwa ufasaha kile kilichotokea kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwezi Oktoba 25 mwaka jana visiwani Zanzibar na mwelekeo wa Demokrasia Tanzania kwa ujumla na Uhuru wa kujieleza una vyominywa na utawala wa Magufuli.

Siku: Jumamosi tarehe 18 Juni, 2016.
Wakati: Kuanzia saa tisa jioni mpaka saa moja usiku kwa majira ya Marekani ya Mashariki.

Mahali: Tabeer Langley Park. Adress 1401 University Blvd E
Hyattsville, MD 20783

Usingoje kuhadithiwa au kusoma maelezo yaliyopotoshwa, njo mwenyewe na maswali yako na yatajibiwa bila utata.

Nyote Mnakaribishwa

10 comments:

MENSA AMANI DMV said...

Watanzania au wafuasi wake toka Pemba na watu WA CUF DMV? Hatuna haja na handouts zake. Hapa DMV na wasomi wengi tunaoishi Marekani tunajua tamaa zake huyu ndugu. NOTHING WILL BE GAINED BY ATTENDING THE SO-CALLED MEETING, PERIOD. LENGO LAKE NI KULETA VURUGU NCHINI, PROVE ME OTHERWISE. Tafadhali mheshimiwa utuache Wana DMV tuendelee kufunga kwa AMANI.

Anonymous said...

Maalimu Seif alitegemea nini wakati alopowazuia wanachama wa CUF wasishiriki uchaguzi wa marudio? Kwa maamuzi hayo yameondokea bunge la baraza la wawakilishi kuwa la chama kimoja.Hata kama CCM ilipanga kumfanyia figisux2 ili aukose uraisi bado CUF ingekuwa na idadi ya kutosha katika baraza la wawakilishi na kuweza kusukuma agenda zao,na kusimamamia serikali.
Sasa hivi amebakia kulalama kwenye media nani atamsikiliza?

Anonymous said...

Hakuna demokrasia ndani ya chama chake vipi ategemee demokrasia ndani ya Zanzibar? Charity starts at home!

Anonymous said...

Si vibaya kumsikiliza,lakini kwa sasa hawezi kufanya chochote kubadirisha matokeo.sanasana anawatafutia matatizo wapemba na si wa unguja kama wanavyojiita. Jiulizeni kwanza kabla yakushabikia vitu. Ikumbukwe JK alimuweka kizuizini kwa muda wa miaka 5.yeye alitakiwa kuwa mshauli wa chama tu kama kweli ana nia ya mabadiriko na si tamaa za utawala.(Anajua hivyo) alikuwa makamu wa kwanza wa Raid chuni ya mwavuli wa CCM,mbona hakukataa kuwa chini ya Rais wa ccm? Sheria za nchi anazielewa vizuri saana. Au mnadhani anawazidi akina salm Ahmed salm.

Anonymous said...

Nonsense!!! Hata kama nimekosa kazi ya kufanya siku hiyo, afadhali niutumie muda huo kujifunza kucheza miondoko ya bongofleva kuliko kwenda kumsikiliza binadamu anayetawalia na ubinafsi na uchu mkubwa wa madaraka. Mtu yeyote mwenye akili zake timamu atajiuliza na kuling'amua hilo kiulani kabisa! Katika hali ya kawaida, katika karne ya 21, huwezi kuwa mgombea wa chama chako kwa vipindi vitano mfululizo na kuongoza chama chako kwa zaidi ya miongo miwili, kama unaamini kwa dhati dhana ya democracy.

Kwa akili yake mbovu ya kiumla, kiumbe huyu mwenye uchu mkubwa wa madaraka anapozungumzia amani ya Zanzibar anamaanisha yeye kupewa madaraka. Tangu lini amani ya nchi na maslahi ya nchi yakatanguliwa na maslahi ya mtu mmoja? Kama mwana DMV ninayefikiri kwa akili yangu binafsi, isiyokuwa ya kuazimwa, na anayeiishi kwenye taifa lililopiga hatua katika maswala ya democracy, nakushauri uachane na Zanzibar. Tamaa zako zimeigharimu Zanzibar zaidi ya miaka ishirini ya maendeleo na damu nyingi isiyokuwa na sababu yoyote kupotea. Yatosha!

James Bond said...

Nyie kama hamtaki kwenda kumsikiliza huo ni uhuru wenu , mimi si mpemba wala kwetu si ZNZ lakini nakwenda kumsikiliza ndiyo democracy ..tukaneni mpaka mchoke lakini ulimwengu unafahamu ubakaji wa democracy uliotokea ZNZ..

Anonymous said...

Nyie vibaraka wa ccm tu hata mfiche majina yenu na kama unaamini uchaguzi ulikuwa halali Znz au Tz in general basi kuwa mjinga mpaka kesho...Ccm haikushinda Znz hiyo inajulikana in short haikushinda kokote. Kama kujiita wasomi basi mkaombe refund zenu

Anonymous said...

You can label the past election the way you want.Lakinijambo moja unalopaswa kufahamu ni kuwa Maalim Seif hawezi kuupata uraisi popote katika dunia hii.

Anonymous said...

sawa na wewe utakua kibaraka na kukubali ujinga mpaka mwisho wa life ....

Anonymous said...

Mzee mpuuzi huyu