Advertisements

Saturday, June 18, 2016

UTALII WA NDANI WAZIDI KUPATA MASHIKO ,WASOMI CHUO KIKUU SMMUCo WATEMBELEA HIFADHI YA NGORONGORO

Simba jike akiwa amepumzika kwenye nyasi 

Na Dickson Mulashani
Suala la utalii wa ndani limeonekana kupata mashiko baada ya wanafunzi wa chuo kikuu cha Stefano Moshi Memorial University College (SMMUCo) kuhamsika na kuamua kutembelea hifadhi ya taifa ya Ngoro ngoro ili kujionea vivutio vya kipekee vinavyopatikana humo.
Wanafunzi hao wakiwa katika geti la kuingia hifadhi ya Ngoro ngoro 


Akizungumzia safari hiyo mmoja wa wanafunzi hao Emmanuel Kalenzi amesema waliguswa kupanga ziara hiyo kuunga mkono wadau mbali mbali wanaohamasisha utalii wa ndani ili kuweza kuwa mabalozi kwa wengine. “Sisi kama wasomi ndio tunapaswa kuwa mabalozi kwa jamii inayotuzunguka na ili uwe balozi mzuri basi uwe umashajionea kwa macho” alisema.
Nyati dume mwenye umri mkubwa ambaye tayari ametengwa na kundi lake 
Ndege aina ya Cranes nao wanapatikana katika eneo la crater 
Nyumbu akiwa amepumzika mara baada ya kula nyasi 

No comments: