Advertisements

Sunday, August 28, 2016

ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUGONGWA NA GARI

Na Mussa Mbeho,Katavi.

Mwanamke mmoja aliyefahamikia kwa jina la ESTA NASORO mwenye umri wa 36 mkazi wa kijiji cha kanoge kata ya katumba amenusurika kifo baada ya magari mawili kugongana uso kwa uso katika eneo la buzogwe walayani Mpanda Mkoani Katavi.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa jeshi la polisi mkoani hapa Damas Nyanda amesema kuwa ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 4 :25 asubuhi katika eneo hilo baada ya magari hayo kugongana uso kwa uso na kuangukia upande wa pili ambapo alikuwa akipita mwanamke huyo hivyo kupelelea kuvunjika mguu wa kulia.

Kamanda NYANDA ameyataja magari yaliyogongana kuwa ni Toyota wish yenye namba za usajili T.890 DGX na Nissan hard body yenye namba za usajili 903 DFP yaliyokuwa yakiendeshwa na Jenerose Abdulngoda pamoja na Godfrey mpanga ambao wote ni wakazi wa mkoani hapa.

NYANDA ameongeza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa madereva hao kutokana na kutokuwa waangalifu pindi wanapoingia kwenye makutano ya barabara hiyo hali ambayo imekuwa ikipelekea wengi wao kusababisha ajari zisizotarajiwa kwa watembea kwa miguu.

"Hiyo ajali imesababishwa na hao madereva kwa sababu hawako makini na matumizi ya vyombo vyao vya moto hivyo kupelekea kugongana na kusababisha mwanamke huyo kuvunjika mguu wake wa kulia na mpaka sasa mwanamke huyo amelazwa katika hosptali yetu ya wilaya akiendelea kupata matibu zaidi",Alisema kamanda Nyanda.

Aidha kamanda NYANDA amesema kuwa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa zaidi wa ajili hiyo ili kuweza kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria madereva wote wawili waliosabisha kutokea kwa ajili hiyo.

Hata hivyo kamandaNYANDA ametoa wito kwa madereva wote kuzingatia kanuni ,sheria na Taratibu za usalama barabarani ili kuweza kuepusha ajiari za mara kwa mara zinazoweza kuhatarisha usalama wa raia.

No comments: