Advertisements

Monday, August 22, 2016

DC KASESELA AWASWEKA NDANI WALINZI WAWILI KWA KUNYANYASA WANANCHI IRINGA

Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akitembelea katika jengo ambalo lililomwagwa maji na Mlinzi wa Kampuni ya Amazon Seculity na kuwaondoa akinamama walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa waliolazwa Katika Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa.
Baadhi ya watu walioondoka eneo la kusubiri wagonjwa na kukaa nje katika hospitali ya Rufaa ya Mkoani Iringa. 


Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela alipokea wakina mama watatu wakiwa wanatetemeka kwa baridi, wakilalamika kumwagiwa maji ya baridi walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa waliolazwa Katika Hospitali ya Rufaa Mkoani Iringa.

Akinamama hao wengi wao wametoka maeneo ya mbali na hospitali hiyo walimwagiwa na walinzi wa kampuni ya Amazon ambao ndio wamepewa kandarasi ya ulinzi hospitali ya Rufaa ya Iringa. 

Mkuu wa wilaya hiyo alifika hospitali kujionea hali halisi, baadae pia akapata taarifa kuwa jana yake Mlinzi wa kampuni hiyo alimpiga mzee aliyekuwa ameleta chakula katika hospitali hiyo na kumwaga kwa mateke. 

Mkuu wa wilaya aliamuru mlinzi huyo na mwenzake wakamatwe pia mwenye kampuni afike kituo cha polisi haraka iwezekanavyo. "Hali hii imeudhi sana hasa ukiona jinsi wakina mama walivyo nyanyasika wengine vyombo vyao na chakula kuloweshwa maji." alisema Mh Kasesela.

No comments: