Advertisements

Monday, August 22, 2016

PICHA: MICHUANO YA OLIMPIKI RIO 2016 YAFUNGWA KWA SHAMRASHAMRA

Rio imemaliza michuano ya Olimpiki kwa shamrashamra za aina yake, licha ya mvua kuwanyeshea maelfu wanamichezo pamoja na watazamaji waliofika kushuhudia michezo hiyo kutoka maeneo mbalimbali duniani.

Mwenge wa Olimpiki umezimwa katika uwanja wa Maracana nchini Brazil, na kuashiria michuano ya Olimpiki Rio imemalizika rasmi.

Gavana mpya wa Tokyo, Yuriko Koike, ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika wadhifa huo alipokea bendera ya Olimpiki kutoka kwa Meya wa Rio, Eduardo Paes, ikiwa ni kuipokeza Japan jukumu la kuandaa michuano ijayo ya Olimpiki.

   Mwanga wa fataki zilizotumika katika kupamba sherehe hizo ukioneka kwa juu ya uwanja
  Shamrashamra zikiendelea ndani ya uwanja kama inavyoonekana 
 Watumbuizaji wakitumbuiza kwa furaha wakati wa sherehe za kufungwa michuano ya Olimpiki Rio 2016


 

No comments: