Advertisements

Wednesday, August 24, 2016

LIVERPOOL YACHARUKA KATIKA KOMBE LA EFLKikosi imara cha Liverpool kimefanya mauaji kwa Burton Albion na kutinga hatua ya tatu ya Kombe la EFL mzunguko wa tatu, baada ya kuichakaza timu hiyo kwa kipigo cha magoli 5-0.
      Divock Origi akifunga goli baada ya kuunganisha pande kutoka kwa Sadio Mane.

Wekundu hao walianza kuongoza katika dakika ya 15 kupitia kwa Divock Origi kabla ya baadaye Roberto Firmino kuongeza la pili 2-0 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Nathaniel Clyne.
Tom Naylor alijikuta akijifunga mwenyewe na kuipatia Liverpool goli la tatu baada ya mapumziko na kisha baadaye Daniel Sturridge kufunga mengine mawili.
                   Roberto Firmino akifunga goli la pili la Liverpool kwa mpira wa kichwa

No comments: