Advertisements

Saturday, August 20, 2016

MKUU WA WILAYA YA ILALA ABAINI WANAFUNZI HEWA 599 KATIKA SHULE 6


Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari mapema leo ofisini kwake Ilala,jijini Dar wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo ambapo uchunguzi wa wanafunzi wengine hewa bado unaendelea.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akisisitiza jambo wakati alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo, Kulia ni Katibu Tawala wa Wilaya hiyo Bw. Edward Mpogolo.


Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema akifafanua jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Ilala wakati alipotangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema ametangaza kupatikana kwa wanafunzi hewa 599 katika shule 6 za wilaya ya Ilala ambazo hakuzitaja, Mjema amesema baada ya uchunguzi huo kufanyika,wamebainika wanafunzi idadi hiyo,ambapo wahusika wote watachukuliwa sheria ikiwamo na hatua za kinidhamu,kwani hayo ni makosa kama yalivyo makosa mengine

Wilaya ya Ilala ina shule za sekondari za serikali 46 na za sekondari 49 ukiacha shule za taasisi binafsi ,zoezi la ukaguzi bado linaendelea katika shule zote za msingi wilayani humo mpaka Septemba mosi mwaka huu ndiyo litamalizika.

Akizungumzia suala la Madawati mkuu wa wilaya huyo, amewapongeza wadau wote waliochangia madawati mpaka kuhakikisha uhaba wa madawati katika wilaya ya Ilala unakwisha, huku kukiwa na ziada ya madawati 2821

Ameongeza kuwa kazi kubwa inayofuatia kwa sasa ni kuongeza vyumba vya madarasa ambapo kazi hiyo inaendelea vizuri .

Mh. Sophia mjema pia amemshukuru Rais Dk. John Pombe Magufuli kwa kuanzisha mkakati wa wadau kuchangia madawati, jambo ambalo limesaidia tatizo hilo kushughulikiwa kikamilifu na wadau mbalimbali, lakini pia akampongeza Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda kwa usimamizi thabiti wa utekelezaji wa mkakati huo. jambo ambalo limesaidia wilaya ya Ilala kumaliza kabisa tatizo la uhaba wa madawati katika shule za zake za msingi

1 comment:

Anonymous said...

Hivi hii nchi nikipi kilichobaki ambacho si hewa?