Advertisements

Saturday, August 20, 2016

MR NICE APATA MAPOKEZI YA HESHIMA LODWAR, KENYA

 Anaweza kuwa anachukuliwa poa Tanzania, lakini umaarufu wa Mr Nice nchini Kenya bado ni mkubwa na usioweza kuufananisha na mastaa kibao wanaofanya vizuri Bongo kwa sasa (nabii hakubaliki kwao).

Hitmaker huyo wa ‘Fagilia’ amepata mapokezi ya heshima mjini Lodwar, Kenya yanayotaka kushabihiana kidogo na yale aliyoyapata Diamond Platnumz aliyeenda huko miezi kadhaa iliyopita.

Muasisi huyo wa style ya Takeu, atatumbuiza Jumamosi hii kwenye kiota cha MARBLE CLUB & VIP LOUNGE.

No comments: