Advertisements

Saturday, August 20, 2016

CCM WATAKA MAALIM SEIF AZUIWE KUHUDHURIA MATUKIO YA KITAIFA

Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeitaka Serikali kumpiga marufuku Katibu Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Sharif Hamad kuhudhuria hafla na matukio ya kitaifa kutokana na kitendo alichokifanya hivi karibuni kwenye msiba wa Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Aboud Jumbe.

Maalim Seif alikataa kumpa mkono Rais wa Zanzibar, Dkt. Ali Mohammed Shein kufuatia msimamo wa chama hicho wa kutoshirikiana na Serikali Visiwani humo, wakipinga kufutwa kwa matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25 na Kufanyika kwa Uchaguzi wa Marudio uliompa ushindi wa kishindo Dkt. Shein baada ya CUF kuususia.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Zanzibar), Vuai Ali Vuai alisema kuwa ni muda muafaka sasa kwa Serikali kumzuia kushiriki matukio ya kitaifa. Alisema CCM imefadhaishwa na kitendo alichokifanya Maalim Seif na kuwataka watu wote kukilaani.
“Nawaomba watu wasiendekeze sakata hili kwa sababu linamdhalilisha Maalim,” alisema Vuai. “Hatukutarajia kiongozi kama Maalim kufanya kitendo kama kile,” aliongeza.

Hili ni tukio la kwana kwa Maalim kugoma kumsalimia Dkt. Shein. Awali, Dkt. Shein alimtembelea Maalim Seif na kumjulia hali katika hotel ya Serena jijini Dar es Salaam na walizungumza vizuri wakiombeana heri.

CHANZO: MWANANCHI

3 comments:

Anonymous said...

Hii kazi alikuwa anaiweza Julius peke yake.

Anonymous said...

Diplomasia za kipuuzi sana. Ukikataa kumsalimia Dr Shein ndiyo utapata urais?

Anicetus said...

Everyone has the right of freedom of speech and movement.